WILAYA YA MBEYA MJINI – AJALI YA GARI KUMGONGA MPANDA BAISKELI NA
KUSABABISHA KIFO.
MNAMO
TAREHE 04.01.2014 MAJIRA YA SAA 10:55HRS HUKO MAENEO YA MLIMA NYOKA,
KATA YA UYOLE, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA, BARABARA YA
MBEYA/IRINGA. GARI T.437 AQW AINA YA TOYOTA COASTER LIKIENDESHWA NA
DEREVA ASIYEFAHAMIKA JINA WALA ANUANI YAKE LILIMGONGA MPANDA BAISKELI
AITWAYE ASHURA D/O MWINUKA, MIAKA 22, MKINGA, MKAZI WA UYOLE NA
KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. MWILI
WA MAREHEMU
TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI ZA KILA SIKU,(USIPITWEEEEEEEE)
TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI ZA KILA SIKU,(USIPITWEEEEEEEE)
UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. DEREVA ALIKIMBIA
MARA BAADA YA AJALI NA KULITELEKEZA GARI ENEO LA TUKIO. KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED. Z.
MSANGI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO
VYA MOTO KWA KUZINGATIA/KUFUATA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI
KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE
TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE ILI AKAMATWE NA
SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MWENYEWE.
WILAYA YA RUNGWE – KUPATIKANA NA BHANGI.
MNAMO
TAREHE 04.01.2014 MAJIRA YA SAA 20:00HRS HUKO MTAA WA IGOGWE TUKUYU
MJINI, KATA YA KAWETELE, TARAFA YA TUKUYU, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA
MBEYA, ASKARI POLISI WAKIWA DORIA/MSAKO WALIMKAMATA RAYMOND S/O
EMMANUEL, MIAKA 27, KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA KIWIRA ROAD TUKUYU MJINI
AKIWA NA BHANGI KETE 364 NA MISOKOTO 10 SAWA NA UZITO WA KILO 01 NA GRAM
820. BHANGI HIYO ALIIFICHA KATIKA MIFUKO YA RAMBO. MTUHUMIWA NI MUUZAJI
NA MTUMIAJI WA BHANGI HIYO. TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI
ZINAFANYWA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI
WA POLISI AHMED. Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA
KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA
AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANATOA WITO KWA JAMII KUWAFICHUA WATU
WANAOJIHUSISHA NA BIASHARA YA DAWA ZA KULEVYA ILI WAKAMATWE NA SHERIA
ICHUKUE MKONDO WAKE.
[AHMED. Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
No comments:
Post a Comment