Pages

Monday, January 6, 2014

TAMKO LA NIMROD MKONO KUHUSU YANAYOENDELEA CHADEMA NA TUHUMA ZA MH. MKONO KUMPATIA MH. ZITTO MAGARI MAWILI









Nimesikitishwa na jinsi Chama kikuu cha upinzani ambavyo kwa siku za hivi karibuni kimeingia katika migogoro ambayo inaathari kubwa kwa ustawi wa demokrasia hapa nchini.

Nimesoma kwenye mitandao ya kijamii kuhusu mimi Mh. (Nimrod Mkono) kumpatia Zitto Kabwe (MB) magari mawili (Land Cruiser pamoja na Nissan Patrol).

Kwanza napenda ifahamike kwamba sijawahi kumpatia Zitto magari. Isipokuwa kuhusu hiyo Land Cruiser; nilitoa msaada wa kuwanusuru kule Tarime kwenye msiba wa marehemu Chacha Zakayo Wangwe (MB) Tarime. Wakiwa wanatishiwa kupigwa (Freeman Mbowe pamoja na Zitto Kabwe) nilijitolea gari langu lenye bendera ya Bunge, liwachukuwe na kuwapeleka Mwanza wakiwa salama, na ilifanyika hivyo.


TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI ZA KILA SIKU,(USIPITWEEEEEEEE)
Baada ya kufika Mwanza, Mhe. Zitto aliwasiliana na mimi, kuhusu ununuzi wa gari hilo, nami kupitia kwa wakala wangu Africariers; nilimuuzia Zitto hilo gari.

Kuhusu hilo gari la pili: (Nissan patrol) Mhe. Zitto Kabwe alilikodi, na mpaka sasa anaendelea kulipa vizuri tu; lakini pia ifahamike kwamba hata nyaraka za gari hilo bado ninazo mimi kama mmiliki halali na sijawahi kuhamisha umiliki wake (Transfer of ownership)

KUHUSU KUTOA FEDHA KWA CHADEMA

Nimesikitishwa na ninataka kuweka wazi kwamba, sijawahi kuongea na Tundu Lissu kama inavyodaiwa kwa masuala yoyote binafsi isipokuwa tukiwa kwenye kamati ya Katiba na Sheria.

Ikumbukwe kwamba, nimepita bila kupingwa kwa vipindi vitatu mfululizo (2000, 2005 na 2010). Ni historia ya aina yake; lakini pia uchapakazi wangu kwenye jimbo la Musoma vijijini. Ushindi wangu wa kupita bila kupingwa kwa kiwango kikubwa umekuwa unatokana na bila shaka umahiri wangu kwa kufanya kazi za wananchi kwa kiwango kikubwa

No comments:

Post a Comment