TANGAZO TOKA KWA MKURUGENZI WA MANISPAA YA KINONDONI KWENA KWA WAZAZI WOTE AMBAO WATOTO WAO WAMEFAULU LAKINI WAMEKOSA NAFASI.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni anawatangazia Wazazi
wote wenye watoto waliofaulu mtihani wa Darasa la saba na kukosa nafasi
ya kujiunga na kidato cha kwanza na ambao wako tayari kujiunga na
Sekondari zenye nafasi nje ya Kata zao na Mji wa Kinondoni waende
wakajaze fomu kwa Waratibu Elimu Kata. Manispaa ya Kinondoni
ina nafasi 2102 katika Sekondari za Goba, Fahari, Kibwegere, Kinzudi,
Kwembe, Luguruni, Mabwe, Malamba Mawili, Mbopo, Mbweni na Njechele.
Mwisho wa kupokea maombi ni siku ya Ijumaa tarehe 10/01/2014.
No comments:
Post a Comment