Pages

Wednesday, January 29, 2014

TASWIRA ZA MAKUNGA, KIBANDA BAADA YA KUSHINDA KESI YAO YA UCHOCHEZI KISUTU LEO

Mhariri Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari (2006), Absalom Kibanda akiongea na waandishi baada ya kushinda kesi katika Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu.
Wakili wa washitakiwa, Nyaloni Mwita akiongea na waandishi wa habari nje ya mahakama.
Meneja Uendeshaji Biashara wa Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd (MCL), Theophil Makunga akiongea na wanahabari baada ya kushinda kesi Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communication Ltd,Tido Mhandoa kiongea na waandishi wa habari baada ya hukumu.
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam leo imetoa hukumu ya kesi ya makala iliyodaiwa kuwa ya uchochezi iliyokuwa inawakabili Meneja Uendeshaji Biashara wa Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd (MCL), Theophil Makunga, Mwenyekiti wa zamani wa Chadema Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba na aliyekuwa Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Tanzania Daima ambaye sasa ni Mhariri Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari (2006), Absalom Kibanda ambapo wameibuka kidedea baada ya ushahidi upande wa mashitaka kutojitosheleza. (PICHA: DEOGRATIUS MONGELA NA NYEMO CHILONGANI/GPL)

No comments:

Post a Comment