Bill de Blasio, Mayor mpya wa New York siku ya pili toka aapishwe kuanza
kulitumikia jiji la wasilo lala New York, Sasa ana kumbana na storm ya
theluji mtihani wake wa kwanza kuhakikisha jiji linakuwa safi ndani ya
masaa 24 na watu waendelee na shughuli zao kama kawaida. Kutokana na
theluji jiji la New York shule zimefungwa hadi jumatatu na usafiri wa
ndani ya jiji utakuwa slow kutokana na gharika hilo la theluji itakayo
fikia 6" hadi 8".
Katikati ya jiji la New York eneo la Times Square hali ilikuwa kama hivi
watu wakitembea juu ya theluji, Wakiwa wameshikana kimaloveydavey bump
to bump.
Kutoka na hali ya hewa hii ndege zimestopisha safari na shule za serikali kufungwa.
Hali ya hewa hii ya theluji ilisababisha kuwa na upepo mkali pia kama
unavyoona mwamvuli huu hapa ukinesa nesa kutoka na upepo huo.
Licha ya hali ya hewa hiyo lakini watu hawakushindwa kuonyesha upendo
wao kwa kuandika maneno haya juu ya theluji kuwa wanalipenda jiji la New
York licha ya kupigwa na baridi.
Brooklyn Bridge ni daraja refu linalounganisha Manhattan na Brooklyn kama unavyoona kutoka na storm hiyo ya theluji.
Mitaa inavyooneka watu wakitembea kwa uangalifu kabisa kurudi majumbani kwao hii ilikuwa eneo la Lower Manhattan New York.
Dada akijipiga ukodak mwenyewe wakati theluji ikinyesha
Licha ya theluji hiyo lakini watu waliendelea na kazi ya kuwapelekea
watu chakula majumbani mwao kama unavyoona mtu huyu akiwa na baiskeli
akikata mitaa juu ya theluji.
Magari maalum ya city yakisafisha theluji yakipiga kazi
Kwa juu majengo yakiwa na theluji na magari yakifunikwa na snow pia, hii ilikuwa First Avenue New York.
Unaweza kudhania kuwa inapendeza lakini baridi hiliyopo hapa siyo
mchezo. Magovernor wa New York na New Jersey wameomba watu kukaa
nyumbani bila kutoka kwani hali ya hewa itakuwa baridi sana kuanzia
usiku wa january 2 hadi january 3. Kama una mahindi yako wewe choma tu
taratibu nyumbani kwako.
Barabarani magari yanatembea kwa speed ya harusi kutokana na hali ya hewa hiyo.
Mayor wa New York bwana Bill de Blasio akitoa maagizo kwa mkuu wa kitengo cha kusafisha snow hiyo.
Kachanga chenye umri wa miezi miwili kakiwa kamefunikwa gubi gubi ili kasije nyeshewa na theluji.
Jamaa anawaisha msosi kwa mteja maana walio wengi kupika ni sawa na
kuona snow kipindi cha summer. Mezani kumejaa menu kuliko vijiko vya
chakula duh....
Mama akiwa na chakula chake tayari kwa kutokutoka kesho.
inapendezaje utadhani ni unga kumbe theluji hiyo.
Mambo yamekuwa mambo jamaa gari likamshinda akajikuta amesha lala chali juu ya theluji.
Huyu nae ndiyo anajikongoja
Theluji ni hatari sana inaweza kukusababishia majanga kama haya.
Mama kajizatiti vilivyo ilikujikinga na baridi ya theluji hiyo.
Huyo mtoto ameona ndiyo sehem ya kujifundishia kuski.
No comments:
Post a Comment