Jake Schellenschlager wa Maryland, Marekani, mwenye miaka 14 alianza kufanya mazoezi ya kunyanyua vitu vizito akiwa na miaka 12.
Mpaka sasa anauwezo wa kunyanyua vitu vyenye uzito mara mbili ya uzito
wake, na ndoto zake ni kuja kuweka rekodi ya kunyanyua vitu vizito akiwa
na umri mdogo.
Jake ameiambia Washington Post kuwa alianza kufanya mazoezi baada ya
kumuona baba yake akifanya mazoezi ya kunyanyua vitu vizito katika
garage ya nyumba yao, mpaka sasa hufanya mazoezi kila siku.
Mpaka sasa Jake amefanikiwa kuweka rekodi ya mashindano kadhaa ya
kunyanyua vitu vizito kwa watu wa umri wake, ikiwemo ‘Powerliftng Bench
Press Championships’ iliyofanyika York, Pennsylvania.
Baba yake alisema kuwa kuna baadhi ya watu wanaamini kuwa sio vizuri kwa
watoto wa umri mdogo kunyanyua vitu vizito, na kuongeza kuwa Jake
hajawai kulalamika juu ya maumivu na huangaliwa afya mara kwa mara.
Like father like son, Jake na baba yake
No comments:
Post a Comment