Aliyekuwa
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zitto
Kabwe (kulia) akitoka katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam
leo, ambapo aliwasilisha ombi la pingamizi la yeye kutojadiliwa kwenye
kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho kinachotarajia kufanyika kesho, hadi
rufaa yake ya kupinga kuenguliwa wadhifa huo kwenye Baraza Kuu la chama
hicho. Kushoto ni Wakili wa Zitto, Albert Msando. Mahakama Kuu
imekubaliana na Zitto Kikao cha Kamati Kuu ya Chadema kinachotarajiwa
kufanyika kesho kutomjadili kwa namna yoyote.
Zitto Kabwe akiingia mahakama Kuu Dar es Salaam leo
Wanasheria wa Chadema, Tundu Lisu (kushoto) na Peter Kibatala waliofika kupinga hoja hiyo mahakamani.
Tundu Lisu na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema wakijadiliana jambo wakati wakisubiri uamuzi wa mahakama
Zitto
ana wakili wake Msando wakiwasiliana na marafiki zao walipokuwa
wakisubili uamuzi wa mahakama, ambapo Zitto aliibuka dedea kwa pingamizi
lake kukubaliwa hivyo kikao cha Kamati Kuu kinachofanyika kesho
kukatazwa kumjadili kwa namna yoyote Zitto.
PICHA NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
No comments:
Post a Comment