Sasa wasanii wa Tanzania wameanza kusogeza mbele maisha kwa kuwa wabunifu katika Nyanja ya kutoka kimaisha,
wapo wanotegemea muziki tu au filamu tu lakini tumekuwa tukimwona bwana
mdogo Diamond amekuwa akifanya vitu vingi tofauti na mziki vya kumfanya
aendelee kuwa juu katika sanaa yake. Alie mezani kwetu LEWIS MBONDE
BLOG ni msanii Dr.CHENI ambaye yeye tofauti na uigizaji pia ni
mshehereshaji(MC) amekuwa kivutio kikubwa sana katika shughuli za
masherehe ya kutosha, Cheni ameuambia mtaandao wetu kuwa huwa anapokea
simu nyingi sana za kumhitaji kufanya sherehe kama MC na yuko tayari
wakati wowote anapohitajika maana yeye yupo kwa ajili ya jamii.
Ukimhitaji wasiliana nasi tutakupa mwongozo ili
sherehe yako ifane.
Ukimkaribisha Cheni jiandae kufurahia sherehe yako.
Ni Mshehereshaji mzuri sana asiye na malingo, popote anapoalikwa kuwa MC yeye huwa tayari.
No comments:
Post a Comment