Pages

Monday, January 6, 2014

UNITY ENTERTAINMENT CHINI YA AY WAJA NA WASANII WAPYA WAWILI


MKALI wa muziki wa kizazi kipya, Ambwene Yesaya ‘AY’(Pichani), amewapa shavu vijana wawili wenye vipaji vya kuimba na kuwaingiza kwenye ‘lebo’ yake ya Unity Entertainment.

AY alifikia uamuzi wa kuwachukua vijana hao, kutokana na uwezo wao wa kuimba waliouonyesha kwenye tamasha la muziki lililofanyika viwanja vya Don Bosco, Oysterbay jijini Dar es Salaam, juzi.

Akitangaza nia yake hiyo, AY alisema kuwa aliamua kutumia tamasha hilo lililoandaliwa na Radio Clouds Fm kutafuta vipaji.

Alisema kuwa amevutiwa na uwezo wao wa kuimba, pumzi, sauti pamoja na mwonekano wa kisanii waliokuwanao.

“Mimi kama mmoja kati ya wasanii wa muda mrefu, naona kuwa kwa sasa natakiwa kuwasaidia na wasanii wengine kuwainua, hasa mwanzo huu wa mwaka 2014 nataka kuwafikia vijana wengi zaidi,” alisema AY.


TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI ZA KILA SIKU,(USIPITWEEEEEEEE)
Aliongeza kuwa anaona fahari kwake kuwasaidia vijana kutimiza ndoto zao katika sanaa, kwa kuwa hata yeye pia alisaidiwa.

Alisema kuwa atawalipia gharama za studio kuanzia kurekodi nyimbo zao pamoja na video.
Vijana waliochaguliwa ni mwanadada Florida Moses na Salum Athuman.

Katika tamasha hilo lililofana, kulikuwa na wasanii wengine wakiwamo Madee, Rich Mavoko, Kala Jeremiah, Young D, Young Killer, Dogo Janja na wengineo.
- Tanzania Daima

No comments:

Post a Comment