Pages

Wednesday, January 8, 2014

VIONGOZI WA KITAIFA AKIWEMO RAIS KIKWETE WADAIWA KUDAGANYWA KATIKA MAZISHI YA DR MGIMWA



Hili ni gari  la JWTZ lililobeba mwili wa  waziri Dr Wiliam Mgimwa  kutoka uwanja wa Ndege Nduli hadi kijiji cha Magunga nyumbani alikozaliwa
Ndege aliyotumia  rais  Dr Jakaya  Kikwete ikitua  uwanja wa ndege nduli Iringa
Msafara  wa waziri mkuu Mizengo Pinda  ukiwasili  uwanja waNdege Nduli  Iringa
Mafundi  wa mahema  wakiendelea na ujenzi wa mahema  hayo
Mafundi  ujenzi  wakijenga kaburi la Dr Mgimwa ambalo linadaiwa  kutumia kiasi cha Tsh milioni 3
Barabara  iliyetengenezwa kwa ajili ya ugeni wa kitaifa   japo eneo hilo la barabara ya Masumbo - Kiponzero lilikuwa korofi  siku nyingi

SIKU  mbili  baada ya mazishi  ya aliyekuwa  mbunge wa jimbo la Kalenga Dr Wiliam Mgimwa ambae  pia alikuwa ni waziri wa  fedha wananchi  wa jimbo hilo wameipongeza  serikali kwa  kukarabati maeneo korofi ya  barabara ya Masumbo - Kiponzero ili  kuwezesha viongozi  wa kitaifa akiwemo Rais  kupita bila  tatizo.
Zebedayo Kalinga ambae ni mkazi wa Kiponzero  alisema  kuwa  msiba  huo na kama na  ule usemi wa kufa kufahana  kutokana na serikali ya  mkoa  kujaribu  kuficha kasoro  zote za miundo mbinu  ya kuelekea  weneo la msiba jambo ambalo  wao kama wakazi wa  jimbo  hilo wamefurahishwa na jitihada hizo.
Hata   hivyo alisema wangefurahishwa  zaidi iwapo msafara wa Rais Jakaya  Kikwete ungepita katika barabara ya  Kalenga - Kiponzero  barabara  yenye miundo mbinu mibovu  zaidi  ili kupitia msiba  huo iweze kutengenezwa kama ilivyofanyika  katika barabara ya Masumbo - Kiponzero 
Kwani  alisema kwa  siku nyingi  maeneo ambao yametengenezwa yalikuwa yakisumbua  watumiaji wa vyombo vya usafiri ila kwa  kuwa hakuna  kiongozi  wa kitaifa  aliyepata  kufika  huku suala  hilo  lilifumbiwa macho.
Kalinga  alisema kwa upande wake mbunge wao Dr Mgimwa enzi za uhai  wake amepigania kweli ujenzi  wa barabara na ubovu wa barabara  hiyo ila hakusikilizwa  lakini  baada ya  kifo chake ndani ya  siku  mbili barabara  imetengenezwa .
Hivyo  alisema kama msiba  huo   mwili  huo ungekaa nchini Afrika kusini kwa  mwezi mmoja ama mwaka kulikuwa kuna  uwezekano wa kijiji cha Magunga ambacho  toka nchi ipate uhuru hakijapata maji safi na salama  kupatiwa  huduma  hiyo  ili  kuwafurahisha  viongozi wa kitaifa .
Kwa  upande wake Zuwena Sanga  alisema  kuwa ingependeza   serikali ya mkoa  wa Iringa na Halmashauri ya  wilaya ya Iringa katika kumuenzi mbunge  huyo  kusaidia  kufikisha huduma ya maji na umeme  katika  kijiji hicho kama sehemu ya ahsante Dr Mgimwa kwa utumishi uliotukuka
Pia  alishauri  viongozi  wa ngazi za chini  kuacha  kuficha matatizo ya  wananchi wakati wa ziara za viongozi wa kitaifa kwani kwa kufanya  hivyo ni kuendelea  kuwatesa  wananchi wa pembezeno ambao  siku zote maisha  yao ni tabu ila  viongozi  wa juu wanapowatembelea viongozi wa chini  wamekuwa  wakificha ukweli halisi wa maisha  yao.
Alisema  kutengeneza  barabara  kwa ajili ya  viongozi wa kitaifa ni  sawa na kuwadanganya  viongozi hao ambao  walipaswa  kuona maisha halisi ya  wananchi  wao.picha na habari na Fransis Godwin(Iringa)

No comments:

Post a Comment