Kufuatana na uchunguzi wa maoni ulochapishwa Jumamosi na taasisi ya IFOP, asili mia 41 tu ya wafaransa wanaounga mkono mpango wa serikali kuwaweka wanajeshi wa Ufaransa huko Jamhuri ya Afrika ya kati, kulingana na asili mia moja 51 walounga mkono mpango huo mwezi mmoja uliyopita.
Mchambuzi wa masuala ya kisiasa mjini Paris Mohamed Swaleh anasema "inavyonekana Wafaransa hawaoni faida ya wanajeshi wa nchi yao kubaki nchini humo, kwa vile hakuna adui mmoja wanaopambana nae, na ni vita vya wenyewe kwa wenyewe. Zaidi ya Hayo hawajui mapigano yataendelea kwa muda gani kutokana na hali kwamba mapambano yameongezeka".
TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI ZA KILA SIKU,(USIPITWEEEEEEEE)
Kwa upande mwengine uchunguzi huo wa maoni unaonesha Wafaransa wanaendelea kuunga mkono juhudi za jeshi la Ufaransa huko Mali kutokana na ushindi walopata kuwafurusha waasi wanaoungwa mkono na Al-Qaida, na kurudisha amani na umoja wa nchi hiyo.
Kufuatana na Umoja wa Mataifa zaidi ya watu 900 000 wamekimbia makazi yao tangu mapigano kuanza kati ya wanamgambo wa kikristo na waislamu wa kundi la Seleka lililompindua Rais Francois Bozize mwezi wa April mwaka 2013.
Umoja wa Mataifa unaeleza kwamba mambo yanazidi kuwa mabaya na hadi hivi sasa idara mbali mbali za umoja huo zimewafikia watu elfu 23 pekee yake kuweza kuwapatia msaada. Chanzo: voaswahili
No comments:
Post a Comment