Pages

Wednesday, January 29, 2014

WAKAZI WA WILAYA YA CHAMWINO MANISPAA YA DODOMA WAMETAKIWA KUSHIRIKI KATIKA SHUGHULI ZA MAENDELEO YA SECTA YA ELIMU.


Akizungumza na kituo hiki afisa elimu wa wilaya ya chamwino bi. Scola Kapinga amesema  changamoto kubwa inayo ikabili wilaya ya chamwino  katika Secta ya Elimu ni upungufu wa madawati hususani katika shule za sekondari.
Aidha Bi Kapinga  ameongeza kuwa  mwaka jana walikuwa  na kampeni ya kuwahamasisha wazazi kutengeneza madawati kwaajili ya matumizi ya wanafunzi.
Sanjari na hayo bi Kapinga  amesema kuna baadhi ya  vijiji  katika wilaya hiyo vimeanza kuweka mpango wa kutengeneza dawati moja kwa  kilakaya ambapo mpango huo utarajia kuanza ifikapo mwezi octoba mwaka huu.
 
WAKAZI MKOANI HAPA WAMEPATIWA MSAADA WA CHAKULA KUTOKA NA UPUNGUFU WA CHAKULA ULIO  YAKUMBA BAADHI YA MAENEO.
Akizungumza na Dodoma fm Afisa Kilimo wa mkoa wa Dodoma Bwana Benard Abraham amesema Mkoa wa Dodoma ulipata tani 1672.3  ambapo tani 167.1 ni ya chakula kinacho tolewa bure na tani 1505.2 ni ya chakula kitakacho nunuliwa kwa bei nafuu.
 Aidha Bwana Abraham  amezitaja wilaya zilizonufaika na msaada huo  wa chakula kuwa ni pamoja na wilaya ya Mpwapwa, Dodoma mjini , wilaya ya Kongwa, Chamwino pamoja na wilaya ya  Bahi.chanzo DODOMA FM

No comments:

Post a Comment