Pages

Monday, January 27, 2014

Waziri Kapt Mstaafu George Huruma Mkukuchika awataka watumishi kufuata maadili katika utumishi


index                    Na Kibada  Kibada-Mpanda        
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais  Utawala Bora Kapt Mstaafu George Huruma Mkukuchika amewataka watumishi wa umma na kila mmoja kwa nafasi yake kuzingatia maadili ili  kila katika utumishi wa umma ili kuimalisha utendaji na kuepuka vitendo vya Rushwa ambavyo vinarudisha nyuma maendeleo na kupindishwa kwa haki katika jamii.kuzingatia maadili  ya utendaji kazi ndani ya utumishi huu.

Waziri Mkuchika alitoa kauli hiyo katka hotuba yake akiongea na wajumbe wa kikao cha ushauri Mkoa wa Katavi (RCC) kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano Idara ya Maji Wilayani   Mpanda  Mkoani Katavi mwishoni mwa wiki.

Alisema katika hatua ya makusudi ya kuimarisha mapambano dhidi ya rushwa na kudhibiti utovu wa maadili ya watumishi wa umma,Serikali imeanzisha Kamati za Uadilifu (Itegrity Committees) katika kila wizara, Idara na Wakala zake zote.

Akifafanua zaidi alieleza kuwa kamati hizo zilianzishwa pia katika mamlaka zote za Serikali za Mitaa ,alitoa changamoto kwa  Viongozi kuzitumia ipaswavyo kamati hizo kwa kupokea taarifa za vitendo vya watumishi wasiokuwa waadilifu na kuzifanyaia kazi ikiwa ni jitihada za kuongeza uadilifu katika maeneo ya Kazi.

 Kuhusu Rushwa alisema  kuwa  inapotawala sehemu za Kazi husababisha madhara  mengi kwa jamii na pia misingi ya utawala Bora, madhara hayo yanaweza kuhatarisha uhai na usalama wa Taifa,ikiwa ni pamoja na   kutotimiza utekelezaji wa majukumu ya serikali na kukwamisha utoaji wa haki na husbabisha kuongezeka kwa maovu katika jamii.

Aidha madhara mengine husababisha wananchi kukosa imani na serikali yao na kujichukulia sheria mikononi.,athari nyingine ni kukosekana kwa huduma muhimu za kijamii, kutolewa kwa huduma duni,kuwa na viongozi wasio waadilifu na vilevile husababisha kupungua kwa pato la Taifa na hivyo kupunguza uwezo wa serikali katika kuwahudumia wananchi.

Akasisitiza kuwa kwa misingi hiyo  Viongozi wa dini wanayo nafasi kubwa kuhakikisha wanakemia hali ya ummonyoko wa maadili  na kurudisha maadili  katika misingi yake ya haki akawaomba wasaidiane na serikali  kuratibu vipindi vya dini mashuleni  kwa
Akichangia katika kikao hicho mmoja wa wadau Padri Peter Nguma wa Kanisa katoliki alieleza kuwa vijana kukosa Elimu ya Vpindi Mashuleni inasaidia sana kushusha maadili mashuleni hivyo aliomba serikali irudishe masomo ya dini mashuleni.

Kwa upande wake  Mkuu wa Mkoa wa Katavi awali aliwahimiza watendaji wote kujipanga katika kutekeleza Vipaumbele vilivyopo  katika Mkoa ili kuleta maendeleo katika mkoa.na kuwataka watumishi waumma katika mkoa huo kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma.

Katika kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa aliwahimiza watendaji wa Halmashauri zote mkoani humo kuhakikisha  makusanyo ya ndani yanapatikana kwa kuongeza nguvu katika ukusanyaji wa mapato ya ndani ili Halmashauri ziweze kujitegemea kwa sehemu kubwa katika bajeti yake kuliko kutegemea sehemu kubwa ruzuku.

Aidha akizungumzia kuhusu maeneo ya kuongeza mapato kwa upande wa Halmashauri ya wilaya ya Nsimbo aliwahimiza kuchangamkia fursa ya uwekezaji kwa kushirikiana EPZ walioonesha nia ya kuwekeza katika eneo la maonesho ya Nanenane.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Mpanda Vijijini Moshi Selema Kakoso akizungumzia mtawanyiko wa watu na maeneo kuwa mbali na wananchi katika Wilaya ya Mpanda wananchi wengi wanashindwa kupiga kura kutokana na maeneo kuwa mbali sana na vituo vinavyopangwa kwa ajili ya kupigia kura

No comments:

Post a Comment