Pages

Tuesday, January 28, 2014

WAZIRI MUHONGO AWEKA SAINI LESENI ZA UCHIMBAJI MADINI

1Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Profesa Sospeter Muhongo akisaini moja ya Leseni alizozitoa za uchimbaji Madini. Wanaoshuhudia, aliyesimama ni Kaimu Kamshina wa Madini anayeshughulikia Leseni Bw.  John Mayopa na anayeangalia ni Kamshina wa Madini Paul Masanja.2Mmoja wa Wamiliki Kampuni ya J.S Contractors Bw. Sisti Siyvester Mganga akieleza jambo kuhusu Kampuni ya J.S na namna itakavyofanya kazi. Kampuni hii inatarajia kuzalisha madini  aina ya ‘dimension stone’ na kokoto za ujenzi katika eneo la  Kihangaiko Bagamoyo.3Mwakilishi wa Kampuni Ya Osiris Gold T) Ltd. Bw.Shehzada Walli akimweleza Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Prof esa.Sospeter Muhongo kuhusu Kampuni hiyo. Leseni  iliyosainiwa ya kampuni hiyo itaiwezesha kuchimba madini ya Dhahabu katika eneo la Rwamgaza Geita.
4Mwakilishi wa Kampuni ya Kamal Steel akieleza jambo wakati wa kikao cha kusaini Leseni za Uchimbaji Madini. Kampuni hiyo imepewa Leseni ya kuchimba madini aina ya ‘Marble’ katika eneo la Kidayi Kilosa.
Na Asteria Muhozya
Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Sospeter Muhongo   ameweka saini Leseni tatu za Uchimbaji wa Madini kwa Kampuni zinazotarajia kuzalisha madini aina mbalimbali kulingana na maeneo waliyoomba kufanya shughuli hizo.
Kampuni zilizosainiwa Leseni ni Kampuni ya J.S Construction, inayomilikiwa na Bw. Sisti Slyvester Mganga ambaye ameingia ubia Bw. Nakui Chen Kampuni hiyo yenye Leseni ML 501/2014 ina eneo la ukubwa wa km 0.29. Aidha, shughuli za uchimbaji zitafanyika katika eneo la Kihangaiko Bagamoyo na   Madini yatakayozalishwa ni ‘dimension stone’ na kokoto za ujenzi za granite.
Vilevile, kampuni nyingine iliyowekewa saini ya Leseni ni Osiris Gold (T) Ltd. inayomilikiwa na Watanzania Ezekieli Kihali na Shehdaza Walli leseni namba ML 513/2014. Madini yatakayozalishwa na Kampuni hii ni dhahabu katika eneo la ukubwa wa km 9.94, Rwamgaza Geita
Aidha, Mhe. Muhongo ameweka saini leseni ya uchimbaji wa madini aina ya Marble kwa Gagan S.Gupta, Sameer S.Gupta na Shailesh B.Bhandari ambao wanamiliki Kampuni ya Kamal Steel katika eneo la Kidayi Kilosa. Kampuni hii yenye Leseni ML 514/2014 ina eneo la Km 9.52.
Wakati akitoa Leseni hizo za uchimbaji, amewakumbusha wamiliki wa leseni kuhusu kodi na wajibu wa mwenye leseni katika jamii inayohusika ili wananchi na Taifa waweze kufaidika na rasilimali hizo. Uwekaji saini huo umefanyika katika ofisi za Wizara ya Nishati na Madini, Dare s Salaam.

No comments:

Post a Comment