Pages

Sunday, January 26, 2014

WEZI WAIBA MILANGO, TAA ZA GARI NA KUWAPORA WAPITA NJIA BAADA YA KUTOKEA AJALI ENEO LA TANDALE JIJINI DAR

 Nissan Patrol namba T479 BPJ baada ya kuigonga Bodaboda eneo la Tandale kwa Bonge, Dar jana usiku.
 WEZI walipora milango, taa za gari na kuwapora wapita njia kufuatia ajali iliyotokea Tandale kwa Bonge jijini Dar es Salaam baada ya gari aina ya Nissan Patrol namba T479 BPJ kugongana na mwendesha Bodaboda ambayo haikujulikana namba zake jana usiku (Jumamosi).
 Dereva na mmiliki wa gari hilo, Alex Mutabazi akiwa amejeruhiwa baada ya kipigo kutoka kwa vibaka.
 Katika vurumai hiyo ambayo ilisababisha msongamano mkubwa wa magari, vijana wa eneo hilo  walitumia fursa hiyo kung’oa milango na taa za gari hilo na vingine vilivyokuwemo ndani yake na baadaye waliendelea kuwapora wapita njia na watu waliokuwa kwenye daladala zilizokuwa zikipita hapo.


  Gari hilo mali ya Alex Mutabazi (59) likiwa limevunjwa kioo cha mbele na vibaka wa Tandale kwa Bonge.
 Dereva na mmiliki wa gari hilo, Alex Mutabazi (59) naye alichezea kichapo kikali kutoka kwa vijana hao. Polisi walifika eneo la tukio na kufanikiwa kuwatia mbaroni vijana kadhaa waliohusika na uporaji huo.
 Hata vitu vilivyokuwa ndani ya gari hilo pia viliibiwa
 Gari hilo likiwa limeondolewa mlango wa nyuma na vibaka
Vioo vya gari hilo vikiwa vimevunjwa.

No comments:

Post a Comment