Algeria
imeanza siku tatu za maombolezi ya kitaifa kufuatia kuuawa kwa watu
sabini na saba kwenye ajali iliyohusiha ndege moja ya Kijeshi Kaskazini
Mashariki mwa nchi hiyo.
Abiria
mmoja alinusurika ajali hiyo iliyohusisha ndege aina ya Hercules C-130
iliyoanguka katika eneo la milima ya Oum al-Bouaghi, ikiwa njiani
kuelekea mji wa Constantine.
Ripoti zinasema hali mbaya ya anga ilisababisha ajali hiyo ya ndege.
Rais wa nchi hiyo Abdelaziz Bouteflika amewasifu wanajeshi waliopoteza maisha yao na kuwataja kama wafia dini wa taifa hilo.
Wengi wa abiria sabini na nane waliokuwa ndani ya ndege hiyo ni maafisa wa kijeshi na familia zao.
Mwanajeshi
aliyenusurika, anaripotiwa kuendelea kupokea matibabu katika hospitali
moja mjini Constantine kufuatia majeraha ya kichwa.
Wizara
ya Ulinzi imesema kuwa imeunda tume maalum kuchunguza ajali hiyo na
kuwa Ahmed Gaid Salah, ambaye ni mkuu wa majeshi nba naibu waziri wa
Ulinzi atazuru eneo la ajali hiyo.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari, wizara ya ulinzi
imesema kuwa hali mbaya ya anga iliyohusisha kimbunga na mvua kubwa ya
barafu ilisababisha ajali hiyo.
Runinga ya taifa ilionyesha picha za ajali hiyo.
Awali
maafisa wa Ulinzi na shirika hilo la habari liliripoti kuwa watu 103
walikuwa ndani ya ndege hiyo lakini idadi hiyo ilipunguzwa hadi watu
sabini na nane.Chanzo BBC Swahili
No comments:
Post a Comment