Pages

Friday, February 21, 2014

AY,TUNDA MAN WAELEZEA SABABU ZA KUFANYA VIDEO NJE YA NCHI

Kumekuwepo na malalamiko ya chini chini kutoka kwa waandaaji(Directors) wa video za muziki wa Bongo na wadau mbalimbali, kuwa wamekua wakifanya kazi na wasanii wa Bongo fleva tangu wanapokua wachanga(underground) kipindi ambacho hawana pesa, lakini wakipata pesa na kuwa maarufu wanakwenda kufanya video zao nje ya nchi.Ambapo wakifika kwa waandaaji hao wanakua kama wanasaidiana kwa kushuti video kali bila tatizo lolote japokuwa inakuwa ya bajeti ndogo, lakini wasanii huwa wanafanikiwa kwa kukubalika kila sehemu ambayo video zao zinafika na kupiga shows kibao zinazo waingizia pesa za kutosha.
Sasa waandaji hao wanasema cha kusikitisha wasanii hao wa Bongo Fleva wakishapiga shoo nyingi na kupata pesa za kutosha wanaenda kushuti video na waandaaji wa nje yanchi, badala ya kurudi kwao ili wafanye video za bajeti kubwa kitu ambacho hata wao wanakiweza.
Wameongeza juwa wasanii hao wanapoenda nje ya nchi kushuti video wanalikosesha taifa mapato, kwani wakifika kule wanalipa pesa nyingi za kushuti video, wanalipia hotel, wanawalipa mamodo, wananunua vyakula, wanafanya shopping ya mavazi, na huduma zote hizo wanakatwa kodi na nchi husika.
Je wasanii wenyewe wanalizungumziaje hilo


No comments:

Post a Comment