Kipre Tchetche akimtoka beki wa kushoto wa Ferroviario, Emidio Matsinhe leo
Wachezaji wa Azam wakimpongeza Kipre Tchetche leo Chamazi
Kiungo mkabaji wa Ferroviario, de Beira akipiga tik tak dhidi ya mshambuliaji wa Azam FC, Brian Umony leo Chamazi
Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
AZAM FC imepata ushindi mwembamba wa bao
1-0 dhidi ya Ferroviario de Beira ya Msumbiji katika mchezo wa kwanza wa
Raundi ya Awali Kombe la Shirikisho Afrika Uwanja wa Azam Complex,
Chamazi, Dar es Salaam jioni hii.
Shukrani kwake mshambuliaji kutoka Ivory
Coast, Kipre Herman Tchetche aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 41
baada ya kutengewa pasi nzuri ya kichwa na Mganda Brian Umony na kufumua
shuti kali.
Mzanzibari Khamis Mcha ‘Vialli’ walikuwa mwiba kwa safu ya ulinzi ya Ferroviario.
Kipindi cha pili, Ferroviario walicharuka zaidi na Azam nao walipoteza nafasi kama tatu za kufunga mabao mwanzoni.
Refa Mutaz Abdelbasit Khairalla na
wasaidizi wake Waleed Ahmed Ali na Aarif Hassan Eltom wote kutoka Sudan
walionekana kabisa kuwapendelea wageni katika maamuzi yao.
Dakika ya 70 beki mmoja wa
Ferroviario aliunawa mpira wazi wazi kwenye eneo la hatari kufuatia
shuti la Kipre Tchetche mbele ya refa, lakini akapeta.
Matokeo hayo yanamaanisha Azam
itakuwa na kazi ngumu katika mchezo wa marudiano wiki mbili zijazo
nchini Msumbiji, wakitakiwa kulazimisha sare ili kusonga mbele.
Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Mwadini
Ali, Erasto Nyoni, Malika Ndeule, Aggrey Morris, Said Mourad, Kipre
Balou, Salum Abubakar, Himid Mao, Khamis Mcha/John Bocco dk61, Kipre
Tchetche na Brian Umony/Jabir Aziz dk81.
Ferroviarrio; William Manyatera,
Zefanis Matsinhe, Emidio Matsinhe, Abrao Cura/Kiki Simao, Edson Morais,
Reinildo Mandava, Valter Mandava/Hery Antony, Antonio Machava, Manuel
Fernandes, Mario Sinamunda na Manuel Correia/Dje Buzana.
Habari na picha kwa hisani ya Bin Zubeiry Blog
No comments:
Post a Comment