Alisema
kuwa mumewe huyo wa ndoa alimuomba aende kumchajia simu barabarani
ambapo alimuacha mdogo wake wa kike mwenye umri wa miaka 13 na mtoto
akiwa anacheza kitandani.
Alisema
mdogo wake alimwambia kuwa alimsukumiza kitandani akitaka kumbaka ndipo
akapiga kelele na kufanikiwa kumchomoka na kukimbilia nje.
Matilda
alisema kuwa baada ya kumwambia hivyo, yeye alianza kukusanya nguo za
mdogo wake ampe ili aende nyumbani kwao ndipo mumewe huyo alipochukua
kisu alichokiweka pembeni ya godoro na kutaka kumchoma nacho yeye.
Hata
hivyo, Mungu mkubwa kwani Matilda alisema kuwa alifanikiwa kukidaka na
kwa vile kilikuwa kibovu mwanaume alibaki na mpini yeye akabaki na kisu
bila mpini.
Dakika
chache baadaye mtoto alizimia hivyo baadhi ya majirani walimkimbiza
katika Hospitali ya Boch iliyopo Kimara-Suka, Dar ambapo alipatiwa
huduma ya kwanza kisha wakampiga X-Ray na kugundua kuna mshipa mkubwa wa
fahamu kichwani ulikuwa umekatika.
Baada ya
hapo alikimbizwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar. Alipofikishwa
aliingizwa kwenye chumba cha upasuaji ili kuokoa maisha yake lakini
ilishindikana kwani alifariki dunia.

No comments:
Post a Comment