skip to main |
skip to sidebar
CHELSEA, LIVERPOOL, ARSENAL WAJIANDAA KUISHTAKI MAN CITY KUVUNJA SHERIA YA "FINANCIAL FAIR PLAY" ILI WAFUNGIWE KUCHEZA CHAMPIONS LEAGUE MSIMU UJAO
Arsenal,
Chelsea na Liverpool wanaweza kutumia kipengele kidogo kwenye sheria ya
"financial fair play' ya UEFA ili kuibania Manchester City haki ya
kucheza katika mashindano ya Champions league msimu ujao.
Kuna
kanuni za kisheria zinazowapa wapinzani haki ya kuwashtaki City kwamba
wamekiuka sheria na kushindwa kufuata sheria ya ya UEFA ya ‘Financial
Fair Play’ (FFP).
Inafahamika na vyombo vya habari nchini
Uingereza vimeripoti kwamba wanasheria wa vilabu kadhaa vikubwa
wanaelewa juu ya suala hili na wanaangalia kwa umakini ya kutumia
vipengele vya sheria hiyo ili kuishtaki rasmi Man City.
Jana
usiku kocha wa Chelsea Jose Mourinho, ambaye timu yake inakumbana na
City kesho Jumatatu, aliituhumu timu ambayo hakuitaja jina kwa kukiuka
sheria ya FFP.
Alisema: ‘Kuna vilabu ambavyo vinafuata sheria ya
FFP vizuri sana lakini kuna baadhi ya vilabu vinaenda kinyume na sheria
hii. Kwangu, jambo hili lipo wazi kabisa. Sisemi jina la klabu au vilabu
- hiyo sio kazi yangu."
Alipoulizwa
kama ni City ndio waliovunja sheria hiyo na wapo kwenye kuchunguzwa na
UEFA, aliongeza: "Ni kazi ya Mr. Platini na watu wengine kujua hilo, sio
yangu…Nasubiria watafanya nini."
FFP inaelekeza vilabu visipate hasara isiyozidi kiasi cha £37million kwa misimu ya 2011-12
na 2012-13 kwa pamoja, vinginevyo basi basi klabu husika itakayoenda
kinyume itakumbana na adhabu ya kufungiwa kucheza katika michuano ya
ulaya miongoni mwa adhabu nyingine. City wiki iliyopita walitangaza
kupata hasara ya £51.6m kwa msimu wa 2012-13 pekee, kwa maana hiyo watakuwa wamepata hasara ya £149.5m ndani ya miaka miwili.chanzo SHAFIH DAUDA.COM
No comments:
Post a Comment