Marehemu Boniface Mnyachibwe Enzi za Uhai wake |
TANZIA
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni inasikitika kutangaza kifo cha Diwani wa kata ya Mbweni Mh. Boniface Mnyachibwe kilichotokea leo ghafla saa tatu asubuhi.
Tunatoa pole kwa familia yake, wakazi wa Mbweni, Wananchi wa Kinondoni pamoja na Chama chake cha CCM.
Mchango wake mkubwa ktk kuboresha maisha ya wakazi wa Mbweni na Kinondoni kwa kujituma na uadilifu kamwe hautasahaulika. Aidha, kifo chake cha ghafla leo wakati jana tulikuwa naye mpaka saa moja na nusu jioni kwenye vikao vya bajeti ni uthibitisho wa uzalendo wake na mapenzi yake kwa anaowawakilisha na Kinondoni kwa ujumla.
Dua zetu na sala zetu ziende kwa familia yake na wote aliokuwa anawawakilisha.
Mungu aipumzishe roho ya marehemu mahala pema peponi..Imetolewa na Manispaa Ya Kinondoni
No comments:
Post a Comment