“Baada
ya kuonekana raia wamefariki kukatokea ushawishi wa kutaka baadhi ya
watu wabebe dhamana ya askari ambao walionekana hawajatekeleza majukumu
yao inavyotakiwa.” Nchimbi
Songea/Dodoma/Moshi. Aliyekuwa
Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi amesema yeye pamoja na
mawaziri wenzake watatu walikubali kuwajibika kutokana na makosa
yaliyofanywa na askari waliokuwa wakitekeleza Operesheni Tokomeza
Ujangili.
Dk
Nchimbi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini (CCM), alisema
kuna uhalifu wa hali ya juu katika mbuga za wanyama, ambao baada ya
miaka 10 unaweza kumaliza wanyama kwenye mbuga hizo.
Akizungumza
na wakazi wa Manispaa ya Songea kwenye Viwanja vya Kiblang’oma, Kata ya
Lizaboni Songea katika kilele cha maadhimisho ya miaka 37 ya CCM,
alisema Serikali ilifanya uamuzi wa kuwasaka majangili na kuwatokomeza.
Alisema katika operesheni hiyo, wananchi wapatao 11 na askari sita waliuawa jambo lililosababisha matatizo makubwa...
“Baada
ya kuonekana raia wamefariki kukatokea ushawishi wa kutaka baadhi ya
watu wabebe dhamana ya askari ambao walionekana hawajatekeleza majukumu
yao inavyotakiwa.”
Alisema
yeye na wenzake waliwajibika baada ya kutafakari kazi inayofanywa na
askari katika nchi hii kwani wanalala usiku na kung’atwa na mbu kwa
ajili ya wananchi, pia wanapambana na majambazi na hata kupoteza maisha
wakati mwingine wakati wakilinda raia.
Hata
hivyo, alimshukuru Rais Kikwete kwa kumpa heshima kubwa ya kumsaidia
katika kipindi cha miaka minane na kuwatoa hofu watu wa Songea kwa
kuwahakikishia kuwa kasi ya maendeleo katika jimbo lake haitapungua.
Uteuzi
wa Dk Nchimbi na mawaziri wengine Khamisi Kagasheki (Maliasili na
Utalii), Shamsi Vuai Nahodha (Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa) na Dk
David Mathayo (Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi) ulitenguliwa mwishoni mwa
mwaka jana baada ya malalamiko ya wabunge kutokana na matatizo
yaliyojitokeza kwenye Operesheni Tokomeza.
CCM Dodoma waishukia Chadema
Mwenyekiti
wa CCM Wilaya ya Dodoma, Paul Luhamo amewataka wananchi wa Dodoma
Makulu kukikataa Chadema kwa madai kuwa viongozi wake wanaendekeza
malumbano ndani ya chama chao.
Akizungumza
katika maadhimisho hayo ya miaka 37 ya CCM katika Kata ya Dodoma
Makulu, Wilaya ya Dodoma Mjini ambayo ni ngome ya Chadema, alitumia muda
mwingi kuwaponda viongozi wa Chadema kuwa hawana jipya tena.
“Naomba
mrudi CCM na kuweni na moyo wa kuchangia michango mbalimbali kwa ajili
ya maendeleo yenu na watoto wenu hata kama Kata hii inaongozwa na
Chadema,” alisema Luhamo.
Moshi wamnadi mgombea
CCM
Manispaa ya Moshi jana kilihitimisha sherehe za kuzaliwa kwa chama
hicho kwa kumnadi mgombea udiwani Kata ya Kiboroloni, Willy Aidan.
Ujumbe
wa viongozi mbalimbali wa chama hicho akiwamo Katibu wa CCM Mkoa wa
Kilimanjaro, Steven Kijazi na Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Moshi
Mjini, Elizabeth Minde walimnadi mgombea huyo.
Katika
mkutano huo uliofanyika eneo la Mnazi, kwa nyakati tofauti walisema
maendeleo yanayoonekana sasa katika Mji wa Moshi yanatokana na sera
makini za CCM.
Kijazi
alisema haihitaji mtu kuwa na shahada kuweza kutambua maendeleo
yaliyoletwa na CCM katika sekta za barabara, maji, afya, umeme na huduma
za jamii tangu Tanzania ipate uhuru mwaka 1961.
Imeandikwa na Joyce Joliga, Sharon Sauwa na Daniel Mjema.
MWANANCHI
No comments:
Post a Comment