Pages

Friday, February 21, 2014

Familia yaishi chooni ni baada ya nyumba yao kuezuliwa na upepo wilayani Hai, Kilimanjaro

 Aziza Mohamed(55)akiwa na mjukuu wake katika choo ambacho hivi sasa wamekigeuza kuwa makazi baada ya mvua iliyoambatana na upepo mkali kuezua nyumba yake wilayani Hai.
 Aziza Mohamed(55)akiwa na mjukuu wake katika choo ambacho hivi sasa wamekigeuza kuwa makazi baada ya mvua iliyoambatana na upepo mkali kuezua nyumba yake wilayani Hai.

 Nyumba ambayo familia ya Aziza Maohamed ilikuwa ikiishi awali kabla ya kuezuliwa na upepo mkali ulioambatana na mvua katika kitongoji cha Kijweni kijiji cha Mijongweni kata ya Machame/Weruweru.
 Sehemu ambayo analala kwa sasa mtoto wa Aziza Mahamed,Sikujua Aloyce.
 Nyumba ya familia ya Aziza Mohamed iliyoezuliwa na upepo mkali ulioambatana na mvua iliyonyesha wiki iliyopita wilayani Hai.
Misaada toka Bonite bottlers ikishishwa
Mabati yakishushwa kijijni hapo
 Mkuu wa kitengo cha mauzo na masoko wa kampuni ya Bonite Bottlers Christopher Loiruk akikabidhi msaada wa bati na chakula kwa mkuu wa wilaya ya Hai ,Novatus Makunga kwa ajili ya wahanga wa mvua iliyoambatana na upepo iliyoezua paa za nyumba huku kaya zaidi ya 1000 zikikosa makazi na chakula
 Mkuu wa kitengo cha mauzo na masoko wa kampuni ya Bonite Bottlers Christopher Loiruk akikabidhi msaada wa bati na chakula kwa mkuu wa wilaya ya Hai ,Novatus Makunga kwa ajili ya wahanga wa mvua iliyoambatana na upepo iliyoezua paa za nyumba huku kaya zaidi ya 1000 zikikosa makazi na chakula
 Choo hicho kinavyoonekana kwa nje.
 Baadhi ya majengo yaliyoezuliwa na upepo katika kitongoji cha Kijiweni wilayani Hai.
Hali mbaya
Mkuu wa wilaya ya Hai ,Novatus Makunga akiteta jambo na katibu wa mbunge wa jimbo la Hai,Richard Mtui.Kulia kwa ni mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Hai,Merikizedeck Humbe.

Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii,Moshi. 
 FAMILIA moja ya watu watatu akiwemo mtoto wa umri wa miaka saba imelazimika kuhamishia makazi chooni baada ya paa la nyumba waliyokuwa wakiishi kuezuliwa na upepo mkali ulioambatana na mvua iliyonyesha wiki iliyopita katika wilaya ya Hai. 
 Familia hiyo ya Aziza Mohamed (55) mwanae wa kiume, Sikujua Aloyce (40) na mjukuu wake wakazi wa kitongoji cha Kijiweni kijiji cha Mijongweni kata ya Machame Weruweru imekuwa ikiishi kwa zaidi ya siku 14 katika choo hicho ambacho paa lake lilisalimika wakati mvua hiyo ikinyesha. 
 Akizungumzia tukio hilo Aziza alisema wakati mvua hiyo iliyoambatana na upepo mkali ikinyesha alikuwa ametoka nyumbani kwake na kwamba baada ya kuona hali imekuwa mbaya akalazimika kukimbia kurudi nyumbani. 
 "Mvua ilivyokuja nilikuwa sipo nilivyoona hali imekuwa ni mbaya na upepo uliokuwepo ikabidi nikimbilie nyumbani ,nikaanza kumtafuta huyu mtoto na baba yake,nikawa na tangatanga nataka nipike sasa vile nashangaa shangaa kutaka kujua mtoto yuko wapi nikaona kidogo nyumba inafunuliwa bati nikiwa humo humo ndani."alisema Aziza. 
 "Kumbe mtoto na baba yake walikuwa wako chumba cha pili Nyumba kubwa ndipo baadae nikamsikia mtoto ikabidi nianze kupiga kelele tokeni huko tokeni huko,ndio wakatoka ikabidi tukimbilie huku chooni tukaja kupumzika mpaka mvua ikaisha ambako tunaishi hadi sasa."aliongeza Aziza.
 Alisema hivi sasa choo hicho wamekuwa wakikitumia nyakati za mchana kwa ajili ya kujisaidia na kwamba ifikapo usiku hulazimika kufunika shimo la choo hicho kwa gunia ,na kisha kuweka matandiko kwa ajili ya kulala. 
 Mengi,Mbowe watoa msaada wa chakula na bati. 
 Mwenyekiti mtendaji wa makampuni ya IPP, Reginald Mengi kupitia kampuni tanzu ya Bonite Bottlers ya mjini Moshi ametoa msaada wa mabati 200,kilogramu 2500 za unga pamoja na kilogaramu 100 za maharage kwa ajili ya kusaidia familia zilizo athirika na mvua hizo. 
 Akikabidhi msaada huo juzi mkuu wa kitengo cha mauzo na masoko wa kampuni ya Bonite Bottlers Christopher Loiruk alisema Mwenyekiti wa makampuni ya IPP,Mengi pamoja na uongozi wa kiwanda umeguswa na tatizo hilo kwa kuona kuwa walioathirika ni watanzania wenzetuhivyo hawana budi kupatiwa msaada. 
 "Kama Bonite Bottlers na Mwenyekiti wetu ,Reginald Mengi tumeguswa na tatizo hili kwa kuona kuwa hawa ni Watanzania wenzetu,wana Kilimanjaro wenzetu,ndugu zeti na tunafahamu matatizo hayapigi hodi, kwa hiyo yanapotokea ni lazima sote tuoneshe uzaledo ili tuweze kusaidiana"alisema Loiruk. 
 "Tumeanza kwa kutoa mabati 200,tuna vyakula unga kilo 2500,na maharage kilo 100 tunaomba muwakilishe kwa waathirika ,tunaomba makampuni mengine na hata watu binafsi waweze kuja kuwasaidia hawa watu ambao hawana mahala pa kukaa na hata chakula."aliongeza Loiruk. 

 Kwa upande wake katibu wa mbunge wa jimbo la Hai,Richard Mtui alisema Mbunge wa jimbo la Hai ,Freeman Mbowe tayari amekabidhi bati 26 kwa familia zilizofikwa na tatizo hilo huku akiahidi kutoa kiasi cha sh milioni 7 ambapo sehemu ya fedha hizo zinatoka katika mfuko wa jimbo wa Mbunge .

No comments:

Post a Comment