Pages

Wednesday, February 12, 2014

IDARA ya Uhamiaji Mkoa wa Mbeya inawashikilia wahamiaji Haramu 62 ambao ni Wahabeshi raia wa Ehtiopia pamoja na Watanzania wawili wakituhumiwa kuingia nchini kinyume na utaratibu.

Afisa Uhamiaji Mkoa wa Mbeya, William Bambanganya akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake


Uhamiaji Mbeya
IDARA ya Uhamiaji Mkoa wa Mbeya inawashikilia wahamiaji Haramu 62 ambao ni Wahabeshi raia wa Ehtiopia pamoja na Watanzania wawili wakituhumiwa kuingia nchini kinyume na utaratibu.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisinin kwake  Afisa Uhamiaji Mkoa wa Mbeya, William Bambanganya alisema watuhumiwa hao wote wameshafunguliwa mashtaka ya kuingia nchini bila kufuata sheria huku Watanzania wawili wakishtakiwa kwa kuhusika kuwasafirisha Wahamiaji haramu.

Alisema wahamiaji hao walikamatwa katika matukio mawili kutokana na kupata taarifa kutoka kwa Watanzania ambao hawapendi vitendo vya kujihusisha na usafirishaji wa Wahamiaji haramu kinyume na taratibu hivyo kukiwezesha kikosi cha Uhamiaji kuwatia mbaroni kirahisi.

Alisema katika tukio la kwanza lililotokea Februari 8, mwaka huu ambapo Jeshi hilo lilipokea taarifa kutoka kwa raia wema zikisema kuna wahamiaji haramu katika moja ya Nyumba za wakazi wa kitongoji cha Mwaka katika Mji mdogo wa Tunduma Wilaya ya Momba mkoani Mbeya.

Alisema baada ya kufika eneo la tukio walifanikiwa kuwakamata Wahabeshi 45 raia wa Ethiopia pamoja na Mtanzania mmoja aliyefahamika kwa jina la Shukrani Sastoni wakiwa katika nyumba ya Elisha Mwazembe  usiku majira ya saa sita.

Aliongeza kuwa Mwenye nyumba hawakufanikiwa kumkamata ingawa Washtakiwa wote walifikishwa Mahakamani na utaratibu wa kumtafuta mwenye nyumba  bado unaendelea huku hatua za kisheria za kutaifisha nyumba hiyo kuwa mali ya Serikali zikiwa zinafanyika.

Alisema tukio la pili lilitokea Februari 11, Mwaka huu majira ya saa 11 asubuhi katika eneo la Mbozi ambapo Wahamiaji 17  raia wa nchini Ethiopia walikamatwa wakiwa kwenye gari aina ya Noah lenye namba za usajili T 340 BUP likiendeshwa na Lugano Albert.

Alisema mbinu iliyotumika ni Dereva wa gari hilo kutaka kusimama kwa kificho katika moja ya nyumba iliyojitenga peke yake akidhani pana usalama bila kujua nyumba hiyo inakaliwa na watu na kujikuta wakiwekwa chini ya ulinzi na maafisa Usalama wa Taifa ambao ndiyo waliokuwemo kwenye hiyo nyumba.

Aliongeza kuwa tayari watuhumiwa hao wamefikishwa katika vyombo vya sheria wakisomewa mashtaka ya kuingia nchini bila kibali huku Mtanzania ambaye alikuwa ni dereva akisomewa mashtaka ya kuwasafirisha wahamiaji haramu kinyume cha Sheria huku taratibu za kulitaifisha gari hilo kuwa mali ya Serikali zikiendelea.

Afisa huyo aliongeza kuwa utaratibu wa kutaifisha mali au kitu kinachohusika na Wahamiaji haramu utasaidia kupunguza wimbi la uhamiaji haramu hapa nchini ingawa alikiri kuwepo kwa ongezeko la wahamiaji kwa kipindi cha Mwezi huu ukilinganisha na Mwaka jana.

Alisema Februari 2, Mwaka huu walikamatwa wahamiaji 15 raia wa Burundi ambao walifanikiwa kuwarudisha nchini kwao, na kuongeza kuwa Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Mbeya iko katika Mazungumzo na Uhamiaji Mikoa mingine ili kuangalia mianya wanayopitia kabla ya kufika Mkoa wa Mbeya ambapo wanavuka mikoa mingi kabla ya kufika.

Picha na Mbeya yetu

No comments:

Post a Comment