Pages

Monday, February 24, 2014

INASIKITISHA: MAISHA YA BI AZIZA WA KIJIJI CHA MIJONGWENI ALIYEKUWA AKIISHI CHOONI


 
Safari yangu hii ni kutizama maenedeleo ya Bibi Aziza Mohamed aliyekuwa akiishi chooni baada ya nyumba yake kuezuliwa na mvua yenye upepo mkali ghafla milangoni nakutana na kufuri.
Hata pale nilipomwacha siku ya kwanza kufika ,Chooni ambako bibi huyo alihamishia makazi yake pia kulikuwa na kufuri.
Nikalazimika kwenda kwa mtendaji wa Kitongoji cha Kijiweni Abdul Msuya kupata msaada wa kumpata Bi Aziza na safari ya kumtafuta ikaanza.

 
Njiani tunakutana na maeneo ambayo yaliathirika na maji ,yakiwemo mashamba ya migomba ,mahindi kadharika mpunga
 
Mwenyekiti Msuya alinionesha kila mahala palipo pata athari ya mvua hiyo.
Migomba iliharibika vibaya.
 
Udongo ulizolewa na kupelekwa kwenye mashamba ya Mpunga.
 
Hata ndizo zilizokuwa tayari zimebeba pia ziliharibika vibaya .
 
Hata Bamia ikalazimu kina mama kukata mashina ya bamia na kugeuza kuni.
Tarajio la kuvuna mahindi pia limeingia dosari.
Baada ya safari ya takribani nusu saa kwa mbaali namuona Bi Aziza Msuya .
 
Alikuwa akiotesha maharage shambani kwake.
 
Baada ya kusalimiana ikamlazimu kumalizia kwanza kuzika mbegu kwa mashimo aliyokuwa amechimba tayari
Tukaianza safari ya kurejeas nyumbani kwake kwa kuifuata reli.
 
Safari ilikuwa ni ndefu kiasi .
Mwendo ukaongezeka mwenyekiti wa kitongoji Bw Msuya mbele ,Bi Aziza nyuma.
 
Dakika 45 zinakamilisha safari yetu na hatimaye tunafika nyumbani kwa Bi Aziza.
Bi Aziza anachukua funguo na kufungua moja ya chumba katika nyumba iliyoezuliwa na upepo
Ghafla anatoka ndani na furushi ,baada ya kumuuliza hicho nini,kwa unyonge anasema ni matandiko ya mtoto wake Sikujua Aloyce mwenye mtindio wa ubongo.
Anafungua chumba kingine .


 
 Baadae anatoka na fungua ameshikilia mkononi anaelekea kilipo choo.
 Anafungua kufuri la mlango wa Chooni.
Anaingia na kisha anaanza kunifahamisha vitu mbalimbali alivyohifadhi ndani ya choo hicho ambavyo ni pamoja na Nguo zake,zaidi kilichonisikitisha ni uwepo wa Unga na maharage ndani ya choo hicho aliyopewa kama msaada .
Tulizungumza mengi pembeni akiwepo mwenyekiti wa kitongoji cha Kijiweni Msuya akisikiliza kwa makini maelezo ya Bibi zaidi akieleza kuwa alikuwa akiishi katika choo hicho hadi siku hiyo.
Bi Aziza alinieleza kuwa sehemu hiyo ni sehemu ambayo hulala mtoto wake Sikujua ,lakini nyakati za mchana hugeuka jiko.Chumba hiki kipo katika nyumba iliyoezuliwa isipokuwa sehemu ya paa lilibaki na kuweka japo kivuli cha mbali.
Chumba/Jiko.
Bado nikawa na maswali tena hapa chooni kwa Bi Aziza zaidi kuhusu Afya yake hakuona kama ni tatazo.Bi Aziza ananieleza ni tatizo kubwa huku akikiri kuwa ndani ya choo hicho kuna mbu wa kutosha na sasa ameanza kusumbuliwa na MARALIA.
Najaribu kuwaza ,fikiria ni Mama yako uliyemuacha pale kijijini,Bibi yako uliyemuacha kijijini kwenu,Shangaza yako,Mzazi aliyekulea yuko kwenye maisha kama haya  wakati wewe uko mjini ,unauhakika wa kula milo mitatu hadi minne,unawanunulia pombe washikaji ili ujenge heshima ndugu zako pale kwenu kijijini hali yao ni hii,FIKIRIA MARA MBILI.

Natoa pole kwa Bi Aziza kisha naweka mikono yangu nyuma kisha narudi sehemu yangu ya kazi. Naacha hali ikiwa bado haijategamaa ya bibi huyu mkulima. Inaonesha misaada inatakiwa kwake na jamaa wengine wa eneo hili.
Picha na Dixon Busagaga

No comments:

Post a Comment