JESHI la polisi mkoani Iringa linawashikilia watu saba
kwa makosa tofauti tofauti likiwemo la mkazi wa Makongati Tarafa ya Mololo
aitwaye Mario Kibodya (30) kumbaka mwanafunzi wa darasa la pili jina
limehifadhiwa (8) na kumsababishia maumivu makali sehemu za siri.
Akizungumza ofisini kwake
Kaimu kamanda wa polisi Mrakibu mwandamizi Peter Kakamba alithibitisha kutokea
kwa tukio hilo
lililotokea mnamo tarehe 20 februari majira ya saa 9 kamili mchana.
Wakati huohuo mkulima aliyefahamika kwa jina la Junus
Mkovano (35) mkazi wa Mgama tarafa ya Kiponzero anashikiliwa na polisi kwa kosa
la kumbaka mkulima mwenzake aitwaye Lucy Bahary (41).
Kaimu Kakamba alisema tukio hilo lilitokea mnamo tarehe 20 februari
majira ya saa 1 kamili asubuhi ambapo mtuhumiwa huyo alimvamia mwanamke huyo
akiwa shambani na kumfanyia kitendo hicho na kumsababishia maumivu makali
sehemu za siri.
Mbali na matukio hayo mawili ya ubakaji Kaimu Kakamba
alisema watu watano wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Iringa kwa kosa la kukutwa na madawa ya
kulevya aina ya bhangi misokoto 123.
Kamanda Kakamba alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataja
watuhumiwa hao ni Joseph Lihundi, Justine Mwelungo, Benedict Nzuki, Baraka
Malinga pamoja na Nathani Simon ambao walikamatwa na askari wakiwa doria maeneo
ya Makorongoni.
NA DIANA BISANGAO WA MATUKIO
DAIMA.COM, IRINGA
No comments:
Post a Comment