Pages

Friday, February 14, 2014

JIMBO LA TEMEKE CCM LAFANYA UCHAGUZI WA VIONGOZI




 Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu akimkaribisha Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, alipowasili kwenye ukumbi, baada ya kuwalikwa kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Jimbo hilo, ambao uliambatana na uchaguzi wa Mwenyekiti wa Jimbo na Katibu ambapo katika jumla ya kura 54 zilizopigwa Ahmad Mnamala alipata kura 50 za ndiyo na tatu za hapana na hivyo kuibuka mshindi, huku kwa jumla ya kura hizo hizo zilizopigwa, Kasim Kiame akiibuka kuwa Katibu wa jimbo kwa kupata kura zote 54 za ndiyo.

 Sjeikh Salum akisalimiana na Mtangazaji wa Channel Ten, David Ramadhan
 Shekh Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, akisalmiana na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Temeke, Sikunjema Shabani, baada ya kuwasili ukumbini.
 Mtemvu, Sheikh Salum na Mwenyekiti wa CCM wilaya wakishangilia kabla ya kukaa vitini kuruhusu kikao kuanza
 Wajumbe nao wakiwa wamesimama kuwalaki viongozi wa meza kuu
 Meza ya ufundi ikiwa kazini kuhakikisha itifaki zote zinakwenda sawa
 Sheikh Salum akizungumza mwanzoni mwa mkutano huo ambapo alisisitiza msimamo wake kuwa yeye ni Muumin wa serikali mbili na kuwataka wajumbe wa mkutano huo nao kuamini hivyo. Pia aliwatakia uchaguzi mzuri wakimtanguliza Mungu mbele ili kumpata kiongozi atakayelisaidia jimbo hilo la Temeke
 Sheikh Salum akishikana mkono na Mtemvu baada ya kuzungumza
 Mwenyekiti wa CCM wilaya aya Temeke akizungumza
  Ahmad Mnamala akiomba kura kwa wajumbe wakati akijieleza
 Kasim Kiame akiomba kura za kuwa katibu wa jimbo
 Wajumbe wakigawiwa karatasi za kura

Baadhi ya wajumbe wakipiga kura.PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

No comments:

Post a Comment