Pages

Thursday, February 13, 2014

KAMANDA WA POLISI MKOA WA DODOMA DAVID MISIME - SACP AKUTANA NA WAFANYABIASHARA WAMILIKI WA HOTELI NA NYUMBA ZA KULALA WAGENI MKOANI DODOMA

 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma DAVID MISIME - SACP akiongea na wafanyabiashara wamiliki wa Hotel na nyumba za kulala wageni mkoani Dodoma..
 Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Dodoma 
FAUSTINE MWAKALINGA akiongea na wafanyabiashara wenzake
 Mwenyekiti wa wenye mahoteli na nyumba za kulala wageni mkoa wa Dodoma CHAVUMA TARATIBU akielekeza jambo katika kikao hicho cha wafanyabiashara Mkoani Dodoma.
 MOHAMED NTEMO (Com.Ntemo) akichangia
 jambo katika kikao hicho cha wafayabiashara Mkoani Dodoma
 Baadhi ya wafanyabiashara wamiliki wa Hotel na 
nyumba za wageni katika mkutano huo
 Baadhi ya wafanyabiashara wamiliki wa Hotel na
nyumba za wageni katika mkutano huo
****************
Na Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma. 
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME (SACP) amewataka wamiliki wa Hotel na Nyumba za kulala wageni (Guest House) kuhakikisha kwamba wageni wanaotarajia kuingia mkoani humo ambao ni wajumbe wa bunge la Katiba linalotarajia kuanza tarehe 18/02/2014 wanakuwa salama katika kipindi hiki. 
 Amesema hayo katika ukumbi wa Dodoma Hotel alipokuwa akizungumza na wafanyabiashara ambao ni wamiliki wa Hotel na Nyumba za kulala wageni Mkoani humo na kusisitiza kubandika namba za viongozi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma ili kuweza kutoa taarifa za kihalifu pamoja na kupata huduma haraka ya kipolisi. 
 Pia Kamanda MISIME amesema kulingana na kukua kwa sayansi na teknolojia amewashauri wamiliki wa nyumba hizo kwa baadaye waboreshe huduma zao kwa kufunga CCTV – Camera kwenye korido, kaunta na nje ya Hotel na nyumba zao ili kuweza kurekodi na kutunza kumbukumbu za matukio katika maeneo yao ya biashara. 
 Aidha Kamanda MISIME amesema ni lazima wamiliki wa Hotel na Nyumba za kulala wageni waweze kubaini changamoto zinazowakabili na kutathimini kila mmoja kama eneo lake linausalama kwa kiasi gani ikiwa ni pamoja na kufuata sheria zote za Hotel na nyumba za kulala wageni. Halikadhalika Kamanda MISIME amewataka wamiliki hao kushirikiana katika kupunguza ajali za usalama barabarani pamoja na kujenga utamaduni wa kusema familia yangu haina uhalifu. Kamanda MISIME amesisitiza kuwa wageni wote watakaofika katika nyumba za kulala wageni wajazwe katika vitabu vya wageni, na kama wapo wawili asiondoke mmoja mpaka kwa ruhusa ya mwenzake kitu kitakachoweza kubaini uhalifu utakaoweza kujitokeza. 
 Vilevile ameongeza kwa kusema wahudumu wa nyumba hizo pamoja na Hotel wanatakiwa kuwa makini kwani katika kipindi hiki ndipo matapeli na wezi huwa wakiongezeka kwa kasi. 
 

No comments:

Post a Comment