Pages

Monday, February 24, 2014

Kasisi akiri kulawiti watoto UK


Kasisi mstaafu Francis Paul Cullen,
Kasisi mmoja wa kanisa katoliki mwenye umri wa miaka 85 amekiri kosa la kulawiti watoto wengi pamoja na kuwatendea unyama watoto wengine wasichana baada ya kufukuzwa kutoka katika kisiwa cha Tenerife nchini Uhispania.
Katika kesi iliyokuwa inasikilizwa leo katika mahakama mjini London kasisi huyo, kwa jina Francis Paul Cullen, alikiri makosa 21 ya kuwatendea uchafu watoto saba.
Vitendo cha kuwalawiti watoto wavulana na kuwatendea unyama wasichana, vilitokea kayi ya mwaka 1957 na 1991.
Msemaji wa dayosisi ya Nottingham mjini Uingereza kasisi Andrew Cole alisema kuwa amefurahi kwa kasisi huyo kukiri makosa dhidi yake.
Kasisi Cole alisema kuwa hakuna kinachoweza kuondoa masaibu yaliyowatokea watoto lakini kasisi Cole alisema anatumai kuwa hii itawasaidia kwa njia moja au nyingine.
Cullen atahukumiwa tarehe 24 mwezi Machi.
Alifanya kazi kama kasisi katika dayosisi Mackworth parish ya Christ the King katika mtaa wa Derbyshire kati ya mwaka 1960 na 1978.
Alihamia katika kanisa ya Buxton kuanzia mwaka 1978-87 na kanisa nyingine ya Hyson Green, kati ya mwaka 1988-91.
Alistaafu Septemba mwaka 1991.

No comments:

Post a Comment