SHIRIKISHO
la Soka Afrika (CAF) limeiteua Kenya kuandaa Fainali za Ubingwa wa
Mataifa ya Afrika (CHAN), zinazohusisha wachezaji wanaocheza ligi za
nchini mwao pekee mwaka 2018.Kwa
mujibu wa taarifa ya CAF iliyotumwa leo, hayo yalifikiwa katika kikao
cha Kamati Kuu ya CAF chini ya rais wake, Issa Hayatou, kilichofanyika
Ijumaa ya Februari 21 makao makuu ya bodi hiyo, Cairo, Misri.
“Kamati Kuu ya CAF imeipa Kenya haki za
kuandaa Fainali za mwaka 2018 za ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN),
kufuatia kuhakikishiwa na serikali ya nchi hiyo kwamba watafanya kwa
ufanisi,” imesema taarifa ya CAF.
Kikao hicho pia kimesema Fainali zijazo
za Mataifa ya Afrika (CAN) zitafanyika Morocco mwakani na fainali
zitachezwa kuanzia Januari 17 hadi Februari 7, katika miji ya Rabat,
Agadir, Tangier na Marrakech.
Jumla ya nchi 51 zinatarajiwa kushiriki,
nchi 21 za juu kwenye viwango vya ubora zitaanzia kwenye hatua ya
makundi, wakati nyingine zitaanzia kwenye mchujo.
No comments:
Post a Comment