Mchezo
wa ligi kuu Uhispania kati ya Villarreal ambao walikuwa wanakuwa katika
uwanja wa nyumbani kukipiga dhidi ya Celta Vigo uliahirishwa dakika ya
88 baada ya mabomu ya machozi kurushwa uwanjani.
Celta Vigo walikuwa wanaongoza kwa 1-0 katika dimba la El Madrigal wakati ambapo mabomu ya machozi yalianza kurushwa.
Mwamuzi
David Fernandez alisimamisha mchezo na kuwaambia Wachezaji watoke
uwanjani wakati ambapo mashabiki wengi wao wakifunika macho yao wakianza
kukimbizana.
Mchezo huo ulianza tena baada ya dakika 20 ambapo Celta walishinda 2-0.
No comments:
Post a Comment