Balozi
wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula akiingia ukumbini
siku ya Jumapili Feb. 23, 2014 kwenye sherehe ya maadhimisho ya miaka 37
ya CCM yaliyofanyika College Park, Maryland na kuhudhuriwa na wafuasi
na wanachama wa Chama cha Mapinduzi DMV.
Meza
kuu kutoka kushoto ni Ismail (katibu wa Vijina CCM DMV) George Sebo
(mwanyekiti CCM DMV) Mhe. Liberata Mulamula (Balozi wa Tanzania nchini
Marekani), Mama Kimolo (kitengo cha UWT) na Phanuel Ligate (CCM tawi la
California)
Balozi Liberata Mulamula akiwa meza kuu na mwenyekiti wa CCM DMV George Sebo
Balozi
Liberata Mulamula akiongea na wanaCCM DMV na kutoa historia ya chama
hicho na kuongelea maswala ya mchakato wa rasimu ya katiba kuhusu swala
la raia pacha ukiwemo umuhimu wa bima ya WESTADI kwa ajili ya kusaidia
misiba inapotokea na kuwakumbusha Watanzania Nchini Marekani kuhusu
sherehe ya miaka 50 ya muungano inayotarajiwa kufanyika Kitaifa
Washington, DC April 26, 2014 na kuelezea siku hii ndio siku pekee
inayotambulika nchini Marekani.
Mwenyekiti CCM DMV akiongea machache na baadae kumkaribisha Balozi Liberata Mulamula.
Balozi Liberata Mulamula akisaidiwa na Mwenyekiti CCM DMV kukata keki
Balozi Liberata Mulamula katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa CCM DMV.
Balozi Liberata Mulamula akifungua dansi na wanachama wa CCM DMV akiwemo mwenyekiti George Sebo.
kwa picha zaidi bofya hapa
No comments:
Post a Comment