Pages

Thursday, February 13, 2014

MABASI SITA YA UDA YAPEWA KIBALI CHA KUSAFIRISHA ABIRIA KUTOKA MNAZI MMOJA HADI FERRY

Kutokana na adha wanayopata abiria wanaofanya safari zao kati ya Kivukoni na Mnazi Mmoja, SUMATRA ikishirikiana na kikosi cha usalama barabarani (Kanda maalumu) imerudisha usafiri huo ambapo mabasi ya UDA sita (kwa kuanzia) yatakuwa yanafanya safari kila siku katika maeneo hayo.

Usafiri huu umeanza rasmi  jana  tarehe 12.02.2014 asubuhi, japo kulikuwa na matatizo ya hapa na pale lakini kwa kuwa wote (SUMATRA, Polisi na UDA tulikuwa barabarani tuliweza kurekebisha kasoro hizo kwa pamoja.

Njia zitakazotumika ni kama ifuatavyo:

Kutoka Mnazi Mmoja: Zittanzia Mnazi Mmoja kisha zitakwenda hadi kituo cha Baridi na kuendelea na safari kwa kutumia barabara ya Bibi Titi hadi Maktaba kisha zitaingia kulia kwenda Posta Mpya na kwenda Ferry.

Kutoka Kivukoni (Ferry): Yatatumia njia hizo bali zitakapofika makutano ya barabara za Bibi Titi na Uhuru (Traffic light) zitaingia kulia hadi makutano ya barabara za Uhuru na Lumumba kisha zitaingia kushoto hadi eneo zilipoanzia safari kwa ajili ya kuchukua abiri akwenda Ferry.

Tunatarajia idadi ya mabasi itakuwa inaongezeka kuendana na mahitaji, na nakuli itakayotumia ni shilingi 400/= tu.

Conrad Shio
Afisa Mfawidhi Kanda ya Mashariki

K. Shio

Kny: MKURUGENZI MKUU

No comments:

Post a Comment