Hamis Hashim Liguya akiwa katika Hospitali ya Ganga,mjini Mombai India.
SIKU
chache baada mtoto Hamis Hashim Liguya (13) aliyekuwa akisumbuliwa na
tatizo la kuvimba miguu kuwasili nchini India, jopo la madaktari mjini
Mombai, limesema mtoto huyo alicheleshwa kupewa matibabu kwani
angewezekana kutibiwa mapema.
Jopo la madaktari wakiongea jambo.
Mtoto
huyo aliwasili Uwanja wa Kimataifa wa Coimbatore hivi karibuni na
haraka madaktari wa Hospitali ya Ganga, India walimpokea na kuanza
kumpima vipimo vya awali kabla ya kumfanyia upasuaji.
Kila
daktari katika jopo hilo, alimchukua kipimo chake kisha mwishoni
waliutaja ugonjwa unaomsumbua mtoto huyo unaitwa tuma na umemshambulia
hadi kwenye uti wa mgongo lakini kama ungewahishiwa tiba mapema
Tanzania, isingefikia hatua iliyopo ambayo wanadai uwezekano wa kutembea
ni mdogo hata akapofanyiwa upasuaji.
Madaktari wakikagua X- ray.
“Hili
tatizo lingeweza kuwahiwa lisingeweza kufikia hatua hii,
wamemchelewesha kumpatia matibabu, wangemwahisha mapema na kumpa tiba
sahihi, tatizo lisingefikia hatua hii,” alisema mmoja wa madaktari
ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini.
Mtoto
huyo ambaye ameteseka kwa muda mrefu na ugonjwa huo na madaktari wa
Tanzania kushauri apelekwe India, aliondoka nchini Jumamosi iliyopita
akiwa ameambatana na baba yake mzazi, Hamis Mwiguya na mwandishi wa
Global Publishers, Imelda Mtema.
Kampuni
ya Global Publishers Ltd inayozalisha magazeti ya Ijumaa Wikienda,
Uwazi, Risasi, Amani, Ijumaa na Championi, ndiyo ilikuwa ya kwanza
kuripoti habari za ugonjwa wa mtoto huyo, kisha wakajitokeza wadau na
wananchi wengine kumsaidia fedha ambazo zilimwezesha kwenda nchini India
kutibiwa.
Miongoni
mwa wadau ambao walijitokeza kutoa msaada wa kumtangaza, ni mtangazaji
Hoyce Temu wa kipindi cha Mimi na Tanzania aliyejitoa kumsaidia
No comments:
Post a Comment