skip to main |
skip to sidebar
MANISPAA YA KINONDONI YAJIPANGA KUKUSANYA KODI YA MAJENGO
Manispaa ya kinondoni imejipanga kuhakikisha inakusanya fedha nyingi za
kodi ya majengo kwa kuweka mfumo rahisi kwa walipaji.Akizungumza katika
semina ya iliyohusisha watendaji,wenyeviti wa serikali za
mitaa,wahasibu na watu wengine Meya wa manispaa hiyo Mstahiki Yusuph
Mwenda amewataka watendaji wake wa kata 34,kufanya kazi yao kwa uaminifu mkubwa ili kupata mapato yatakayosaidia shughuli mbalimbali za maendeleo.
Alisema baada ya mamlaka ya mapato Tanzania(TRA)Kukubali kuacha jukumu
la ukusanyaji wa kodi za majengo kuwa chini ya Halmashauri,kinondoni
imejipanga kuweka mfumo rahisi kwa walipaji bila ya kulazimika kwenda
ofisi za manispaa kufanya hivyo.
Benki ya CRDB,au kwa wakala wa
Maxi malipo ambaye ameunganishwa na mitandao mbalimbali ya simu,pia
katika ofisi ya Manispaa wanaweza kupata huduma hiyo.
Katika
ngazi ya vitongoji viongozi wote wa kuchaguliwa wakiongozwa na
mwenyekiti wa serikali za mitaa kazi yao itakuwa ya kuhamasisha huku
watendaji wakihusika na ukusanyaji.
Amewataka wananchi kutoa
ushirikiano na kuwataka wenye nyumba ambao nyumba zao hazijasajiliwa
kufanya hivyo ili waepuke adhabu ya kulimbikiza kodi.
Pia
Mkurugenzi wa Manispaa ya kinondoni Mhandisi Musa Natty pamoja na
kuwataka watendaji watendaji kufanya kazi zao kwa uaminifu mkubwa
aliwatahadharisha watakaoiba watachukuliwa hatua za kisheria.Aliseama
viongoziwa kuchaguliwa(wakiwemo wenyeviti wa serikali za mitaa)kutokana
na ukusanyaji wa kodi hizo za jengo watapata asilimia 7(7%).Imetolewa Na Manispaa Ya Kinondoni
No comments:
Post a Comment