Pages

Friday, February 21, 2014

MANISPAA YA SONGEA YAPATA MSAADA WA GARI LA HUDUMA ZA UKIMWI

SAM_7318[2]Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma Hassan Bendeyeko (kushoto) akimkabidhi ufunguo wa gari jipya lenye usajili namba  DFPA 160 kwa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Naftari Saioloyi (kulia).Gari hilo limetolewa ikiwa ni msaada kutoka   Shirika la Waltereed Program kwa ajili ya kuboresha huduma za UKIMWI .Makabidhiano hayo yamefanyika leo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma SAM_7320[1]Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma Hassan Bendeyeko akiwasha gari hili lililotolewa kwa Halmashauri ya Manispaa ya Songea kwa ufadhili wa shirika la Waltereed Program kusaidia huduma za UKIMWI.Hii ni kuashiria kuwa gari lipo tayari kwa huduma zilizokusudiwa.
SAM_7326[1]Gari jipya lenye namba DFPA 160 lililokabidhiwa kwa Halmashauri ya Manispaa ya Songea kwa ajili ya kuboresha utoaji huduma za UKIMWI.Gari hili limetolewa kwa msaada wa shirika la Waltereed Program linalojihusisha na mapambano ya kudhibiti UKIMWI kwa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.
Picha na Revocatus Kassimba Afisa Habari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Ruvuma


No comments:

Post a Comment