![]() |
Mawaziri Ali Juma Shamuhuna na Shukuru Kawambwa wakiongoza mkutano ulowashirikisha maofisa kutoka Wizara hizo jana.
|
![]() |
Waziri wa Elimu na Ufundi wa Tanzania Bara, Shukuru Kawambwa akizungumza kwenye kikao hicho jana. Picha na Martin Kabemba.
|
Story by: Donald Martin Kabemba.
Waziri wa Elimu na Ufundi, Shukuru Kawambwa na Waziri wa Elimu na
Mafunzo ya Amali Zanzibar, Ali Juma Shamuhuna kwa pamoja wamekutana
kujadili mwenendo wa elimu Tanzania na kuchambua matokeo ya Kidato cha
nne hususani viwango vya kufaulu na kufeli na hatimae kuwasilisha
taarifa ya mkutano wao kwenye Baraza la Mawaziri wa Serikali ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Mapinduzi Zanzibar.
Mawaziri hao walikutana jana mjini Zanzibar na kuongea na waandishi wa
habari kuhusu maendeleo na mafanikio ya elimu Tanzania baada ya matokeo
mabaya ya kidato cha nne mwaka juzi ( 2011/2012) Waziri Shamuhuna
alisema kwa upande wa Zanzibar Wizara yake imejizatiti kuhakikisha
vitendo vya udanganyifu katika mitihani vinapungua kwa kutafuta kasoro
zilizojitokeza mwaka juzi na kuzirekebisha.
"Tumekuwa tukizungumza na mabaraza ya mitihani katika shule mbalimbali
ili kuhakikisha hatutarejea pale tulipofanya makosa." Alisema Shamuhuna.
Naye Mheshimiwa Kawambwa amesema baada ya kikao hicho watawasilisha
taarifa maalumu kwa mabaraza ya mawaziri ya Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania. Lakini pia
Waziri huyo amesifu ushirikiano uliopo baina ya Wizara hizo mbili.
" Ushirikiano wetu unazidi kukua siku hadi siku,hili ni jambo zuri kwa maendeleo ya elimu kwa nchi yetu" Alisema Kawambwa.
Wizara hizo mbili zimekuwa na kawaida ya kukutana kabla na baada ya mitihani ya Taifa ili kufanya tathmini ya mitihani hiyo.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment