Mbunge
wa jimbo la Morogoro mjini Aziz Abood akitoa jezi kwa wachezaji wa timu
ya maskani Fc iliopo kata ya Mjimpya mjini hapa.
Mbunge huyo akisalimia na diwani wa kata ya Mindu Hamis Msasa akiteta jambo na mbunge huyo nje ya ofisi ya mbunge huyo jana.
Mbunge wa jimbo la Morogoro Aziz Abood akitoa hundi kwa kikundi cha wanawake cha vikoba cha mjini hapa.
Viongozi
wa kikundi cha vikoba cha wanawake polisi cha mjini hapa wakiwa katika
picha ya pamoja baada ya kupokea hundi shilingi 300,000 kwaajili ya
kutunisha mfuko wao kutoka kwa mbunge wa Morogoro mjini.
mbunge huyo akitoa hundi kwa kikundi hicho cha wanawake polisi
kikundi cha wanawake cha kupika cha Mazimbu mjini hapa wakipokea vyombo vya kufanyika kazi kutoka kwa mbunge huyo
Habari zaidi soma hapa
MBUNGE
wa jimbo l a Morogoro mjini Abdullazizi Abood ametoa msaada wa fedha na
vitu mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 2.53 kwa vikundi
vya wanawake nane vilivyopo katika manispaa ya Morogoro ikiwa ni
kuelekea siku ya wanawake duniani.
Akitoa hundi ya fedha kwa vikundi hivyo
Abood aliwataka wanawake hao kuhakikisha wanatumia msaada huo wa fedha
kwa manufaa ya kujikomboa kiuchumi na kuondokana na utegemezi.
Aidha Abood alisema kuwa kuwapo kwa
vikundi vya wanawake katika maeneo mbalimbali nchini kunalenta
maendeleo ya dhati na hata wanawake kuthaminiwa na waume zao kutokana na
kuongezeka kwa kipato katika familia zao.
“Misaada ninayotoa kwamba nina
fedha sana ila najua majukumu waliyonayo wanawake nchini hasa katika
jimbo langu kwani nimeweza kufanya ziara jimbo langu lote na kujionea
matatizo ya wanawake yanayowakabili,na nia yangu ni kuhakikisha
wanajikwamua na umaskini na kuweza kujitegemea wenyewe”alisema.
Mwenyekiti wa kikundi cha Polisi
Slab vikoba Ukende Ugula akizungumza kwa niaba ya wenzake alimuomba
mbunge huyo kuendelea kutetea haki za wanawake na ,watoto na kuhakikisha
masuala ya wanawake yaliyopo katika rasimu ya katiba yanaingizwa katika
katiba mpya.
Pia alisema kuwa bado kunatatizo la
wanawake wengi hasa wa vijiji kutojua haki zao,na kumtaka mbunge huyo
kutokata tamaa ya kusaidia wanawake hasa katika mkoa wa Morogoro.
Vikundi vilivyopatiwa msaada ni
Tushikamane,Polisi Slab vikoba,Dirisha la maendeleo kutoka chuo cha
maendeleo morogoro,Tujishike,Changamka,Ushindi,Tushikamane bigwa na
kikundi cha mapishi cha Modeco kilichopatiwa vifaa vya kupikia na kugawa
chakula
No comments:
Post a Comment