Naibu
Waziri wa Fedha Mh;Mwigulu Nchemba akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Momba
Mh'Abiud Saidea kuhusu Changamoto za Ukusanyaji wa Mapato Mpakani
Mwa-Tanzania na Zambia Tundumba,Mkoani Mbeya.Naibu
Waziri wa Fedha Mh;Mwigulu Nchemba akipewa maelekezo kuhusu Upimwaji wa
Viwanja uliofanyika na Halmashauri ya Mbozi Kwenye Mpaka wa Tanzania na
Zambia .
Naibu Waziri akiangalia Jiwe la Msingi la Mpaka lililopo Mpakani Mwa Tanzanzania na Zambia(Getini).
Moja ya Alama ya Mpaka kati ya Zambia na Tanzania lillilopo katikati ya Makazi ya Watu(Watanzania na Wazambia).
Na.
Naibu Waziri wa Fedha Mh:Mwigulu
Nchemba hii leo amefanya Ziara ya Kikazi Wilaya ya Momba(mpya) Mkoani
Mbeya Kuzungumza na Watendaji wa TRA na Wafanyabiashara wa Mji wa
Tunduma mpakani Mwatanzania na Zambia.Katika hatua ya awali Mh:Naibu
Waziri ametembelea maeneo ya Mpaka wa Zambia na Tanzania kuangalia namna
zoezi la Ukusanyaji wa mapato kwa wafanyabiashara linavyokuwa gumu
kutokana na eneo la Mpakani kutumika na Wananchi wa pande zote mbili
kibiashara na makazi jambao linaliporekea.
1.Kushamiri kwa biashara za Magendo hivyo kuliingizia hasara Taifa.
2.Ukwepaji Mkubwa wa Kodi kwa
Wafanyabiashara kutokana na wengi wao kufanya biashara Tanzania na
Wanaishi ng'ambo(Zambia),Wengine ni watanzania wanafanyabiashara zao
ng'ambo ya mpaka(zambia) na Kuishi Tanzania.
Tatizo kubwa linalopelekea Ugumu huo wa
ukusanyaji wa mapato ni kukosekana kwa (freezone) ya kutenganisha
Makazi ya Watanzania na Wazambia.Hivi karibuni Serikali ya Tanzania na
Zambia imeingia kwenye makubaliano ya Kutenganisha mita 50 pande zote
mbili ilikuweka eneo la wazi la mpaka kwaajili ya kudhibiti mapato na
biashara za magendo.
Picha,hapo juu ni(Spot-line) za awali
zinazoonesha mpaka wa Tanzania na Zambia zilizowekwa kwa makubaliano ya
serikali zote mbili.Hivi sasa serikali inajiandaa kulipa fidia kwa
Wananchi wote watakao vunjiwa makazi yao yaliyondnai ya mita 50 pande
zote mbili za Nchi hizi rafiki.
Naibu Waziri Fedha Mh:Mwigulu Nchemba
amesema kwa upande wa serikali itahakikisha inahimiza vikao vya
maridhiano vinavyoendelea vya makatibu wakuu wa Nchi zote mbili(Tanzania
na Zambia) kuhusu kuweka eneo la wazi la Mpaka ilikuondoa changamoto
zinaoendelea sasa za Ukusanyaji wa mapato,Ukwepaji kodi na biashara za
magendo
No comments:
Post a Comment