Serikali
ya Misri imeiomba serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iisaidie
ili irejeshewe uanachama wake katika Umoja wa Afrika AU.
Ombi hilo
limetolewa na Nabil Fahmy, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Misri mara
baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam Tanzania.
Katika
mazungumzo yake na Bernard Membe, Waziri wa Mashauri ya Kigeni na
Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania, Nabil Fahmy amesema wanaoimba
serikali ya Tanzania iisaidie Misri ili irejeshewe uanachama wake katika
Umoja wa Afrika.
Bernard
Membe, Waziri wa Mashauri ya Kigeni na Ushirikiano wa Kimataifa wa
Tanzania amesema kuwa, atawasilisha ombi hilo la Misri kwa Rais Jakaya
Kikwete.
Misri
ilisimamishwa uanachama katika Umoja wa Afrika tangu Julai mwaka jana
baada ya Rais halali wa nchi hiyo Muhammad Mursi kuondolewa madarakani
na jeshi.
Hadi sasa nchi hiyo bado haijarejeshewa uanachama katika Umoja wa Afrika.
Chanzo: kiswahili.irib.ir
No comments:
Post a Comment