William Zelothe Stepehen akiwa ndani ya ndege aina ya Airbus A319.
|
William Zelothe Stepehen ni Mtanzania wa Kwanza Mmasai aliyepewa ithibati ya kuiongoza ndege aina ya Airbus
A319 punde tu baada ya kupokea mafunzo ya urubani yaliyodhaminiwa na
shirika la ndege la fastjet. Alipata mafunzo hayo nchini Uingereza kwa
muda wa takriban miezi miwili na amerudi nchini Tanzania hivi karibuni.
William alikulia Olosipe jijini Arusha ambapo ni nyumbani kwa wazazi
wake.
William
anafananisha anavyojihisi anapoiongoza ndege ya Airbus A319, na wakati
akiwa katika nyumba nzuri ya kifahari na ya kisasa; anaielezea ndege ya
Airbus A319 kama ndege iliyo imara na ambayo imewekewa mifumo mingi ya
usalama. Kwa maneno yake mwenyewe, anasema “Ndege ya Airbus inakulinda
kweli kweli, kama unaifahamu vyema”
William
amewahi kusomea usimamizi wa wanyama pori; alipata mafunzo ya urubani
kwa mara ya kwanza kule Florida Aviation Academy nchini Marekani mwaka
2006 ambapo alipata leseni yake ya usafirishaji kwa ndege. Ingawa ana
umri mdogo, ana uzoefu wa masaa 3,053 ya kuongoza ndege.
Kumwajiri
rubani huyu mtanzania mwenye miaka 28, ni mojawapo ya jitihada za
fastjet za kuhakikisha kuwa kampuni hiyo inaajiri watendaji wazawa
waliobobea katika fani hiyo hapa nchini. Mikakati yao ya kuajiri pia ni
mojawapo ya wajibu wao mpana wa kuwekeza nchini Tanzania. Kwa kila
rubani aliyepokea mafunzo, fastjet imetumia gharama inayokadiriwa
shilingi 49,546,400 hela za kitanzania ambayo ni sawa na 31,027 dola za
kimarekani.
Fastjet
ni shirika jipya la ndege la nauli nafuu Afrika ambalo lilipata umiliki
wa FLY540 na kwa mantiki hiyo likazindua kampuni ya kwanza ya usafiri
wa ndege ambalo linazingatia bajeti. Fastjet, ambayo inaungwa mkono na
mwanzilishi wa Lonrho na easyGroup Bwana Stelios Haji Ioannou,
imetambulisha nauli za kiwango cha chini hadi kiasi cha Tsh32,000 bila
kujumlisha kodi ili kuwawezesha mamilioni ya watu ambao walikuwa
wameshindwa kusafiri kwa ndege, kuweza kusafiria ndege kwa mara ya
kwanza na kuendelea kutumia ndege mara kwa mara. Tangu kuzinduliwa kwake
mwezi Novemba 2012, shirika hili la fastjet limewasafirisha zaidi ya
watu 70,000 na asilimia 99.7 ya safari za ndege zikisafiri katika muda
uliopangwa
No comments:
Post a Comment