Pichani
juu Naibu waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na watoto, Mhe. Dkt.
Pindi Hazara Chana akikagua utoaji wa mafunzo katika Chuo cha Maendeleo
ya Wananchi Munguri, Kondoa, akiwa ameambatana na Uongozi wa Wilaya ya
Kondoa.
Mheshimiwa
Dkt. Pindi Chana akiwa katika ziara hii ya Kikazi alipata fursa ya
kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa na Chuo cha Maendeleo ya
Wananchi Munguri, kondoa ambacho ni miongoni mwa vyuo 55 vinavyotoa
mafunzo ya elimu ya wananchi, ikiwa ni pamoja na mafunzo ya ufundi
stadi, VET
Wakati
wa ziara hii Mhe. Naibu Waziri aliiasa jamii ya Kondoa kutumia fursa
hii kuwahimiza vijana kuja kupata mafunzo na ujuzi mbalimbali utakao
wawezesha kujiajiri na hatimae kupunguza tatizo la ajira kwa vijana, na
hata kiwango cha umaskini katika jamii.
Alisisitiza
kuwa Serikali ina dhamira ya dhati ya kuimarisha utoaji mafunzo katika
chuo hiki na vingine nchini, ili kufikia vijana wengi zaidi na
kutekeleza kwa vitendo Ilani ya CCM ya mwaka 2010.
No comments:
Post a Comment