Juma Luizio 'Ndanda' ameongezwa Taifa Stars |
Baadhi ya nyota wanaotarajiwa kuiongoza Stars dhidi ya Namibia |
Na Boniface Wambura
KAIMU Kocha Mkuu wa timu ya soka ya taifa
ya Tanzania, Taifa Stars, Salum Madadi amewaondoa wachezaji watano wa
Yanga katika kikosi kilichotajwa awali ili wapate fursa ya kuitumikia
timu yao kwenye mechi mbili za Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al-Ahly
ya Misri.
Nafasi zao
zimezibwa na wachezaji Abdi Banda (Coastal Union), Himid Mao (Azam),
Juma Luizio (Mtibwa Sugar), Said Moradi (Azam) na Shabani Kado (Coastal
Union).
Taifa Stars itaingia kambini keshokutwa
(Machi 1 mwaka huu) jioni kwenye hoteli ya Accomondia jijini Dar es
Salaam, na itaondoka Machi 3 mwaka huu alfajiri kwa ndege ya South
African Airways na kurejea nchini Machi 7 mwaka huu saa 8.15 mchana
No comments:
Post a Comment