SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa
(FIFA) limemuidhinishamshambuliaji Mganda, Emmanuel Arnold Okwi kuchezea
klabu ya Yanga ya Dar es Salaam. Katibu wa Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF), Celestine Mwesigwa ametoa taarifa muda huu kwamba, FIFA
imewaandikia barua ikiwaambia Okwi ni halali kuchezea Yanga SC.
“Suala la Okwi limekwisha, ila siwezi kuzungumza zaidi kwa sasa naingia
kwenye kikao, tutatuma taarifa kwa vyombo vya habari baadaye,”alisema
Mwesigwa. TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI MOTOMOTO(USIPITWEEEE)
No comments:
Post a Comment