RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein
--
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dk. Ali Mohamed
Shein, amefanya uteuzi wa viongozi katika taasisi mbalimbali za
serikali. Uteuzi huo ameufanya kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu 53 cha katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.
Walioteuliwa ni Kibibi Mwinyi Hassan ambae anakuwa Ofisa Tawala wa wilaya ya Kusini Unguja, kuchukua nafasi ya Abdulla Ali Kombo ambaye atapangiwa kazi nyengine.
Aidha,
amemteua Haji Machano Haji kuwa Mkurugenzi wa Uendeshaji na Utumishi
katika Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko kuchukua nafasi ya Maulid
Mussa Takrima aliyestaafu kazi kwa mujibu wa sheria.
Wengine
walioteuliwa ni Issa Ibrahim Mahmoud kuwa Mkurugenzi wa Idara ya
Uratibu wa shughuli za serikali katika ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais
wa Zanzibar, kuchukua nafasi ya Ahmad Kassim Haji ambaye hivi karibuni
ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika ofisi hiyo.
Ameir
Makame Ussi ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Sherehe na
Maadhimisho ya Kitaifa katika ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar, kuchukua nafasi ya Issa Ibrahim Mahmoud ambaye ameteuliwa kuwa
Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa Shughuli za Serikali katika ofisi hiyo.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na kusainiwa na
Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Dk. Abdulhamid
Yahya Mzee, uteuzi wa viongozi hao umeanza Febuari 25 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment