SERIKALI imeruhusu mtu yeyote mwenye uwezo wa kuwekeza katika usafiri wa treni ajitokeze, ili kuuboresha.
Naibu
Waziri wa Uchukuzi, Charles Tizeba, alieleza hayo mjini hapa jana katika
kongamano la uwekezaji Kanda ya Ziwa uliokuwa ukijadili mambo
mbalimbali yatakayoweza kunyanyua uchumi wa Kanda ya Ziwa kwa kuzingatia
sekta sita muhimu.
Moja ya
sekta hizo ni ya uchukuzi ambao wawekezaji wa Kanda ya Ziwa walieleza
kuwa ili kuweza kunyanyua uchumi na kuvutia wawekezaji ni lazima kuwepo
na miundombinu mizuri ambayo ni viwanja vya ndege, treni na barabara.
Akijibu hilo,
Tizeba alisema ni kweli kuna changamoto katika miundombinu Kanda ya
Ziwa ikiwa ni pamoja na usafiri wa treni ambao ungesaidia katika
usafirishaji wa mizigo badala ya kutumia barabara ambazo zina gharama
kubwa huku akitolea mfano mtu anaweza kusafirisha kwa sh milioni tatu
badala ya milioni moja au 500,000.
Kutokana
na hali hiyo, alisema serikali inaruhusu uwekezaji katika njia ya treni
kwa mtu kununua mabehewa ya abiria na mizigo na kufanya mazungumzo na
wizara tayari kwa kuanza kazi.
Hata
hivyo alisema hadi ifikapo mwakani, serikali itakuwa imeshaingiza nchini
vichwa vya treni 13, locomotive 50, mabehewa mapya ya abiria 274 na ya
mizigo 990.
Hata
hivyo, alisema hadi kufikia Juni kutakuwa na mabehewa mapya 22 ya mizigo
na pia mabehewa 1,960 yatapatikana ndani ya miaka miwili ya fedha
ijayo.
Akizungumzia kuhusu usafiri wa ndege, alisema atahakikisha anasimamia upanuzi wa uwanja wa ndege wa Mwanza.
“Sio tu
kuurefusha uwanja huo bali hata kutengeneza sehemu ya abiria, tufanye
marekebisho sehemu ya michoro, pia uendelezaji wa uwanja wa ndege wa
Bukoba na kwamba kwa sasa tani 50 zinatua na kuwepo na uwezo wa kushusha
abiria 70 kila siku,” alisema Tizeba.
Kongamano
hilo litatilia mkazo uendelezaji wa sekta ya kilimo, mifugo, uvuvi,
maliasili na utalii, miundombinu, huduma za jamii na nishati, sekta
ambazo zina fursa nyingi katika Kanda ya Ziwa.
No comments:
Post a Comment