Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KATIKA
kukabiliana na uhaba wa walimu nchini serikali imetangaza kuajiri walimu
wapya 36,071 ambapo watapangiwa vituo vya kazi mwezi ujao.
Hatua
hiyo ni mikakati ya serikali katika kukabiliana na uhaba wa walimu
ambapo sasa watakuwa na upungufu wa walimu 21684 kutoka 57755
iliyokuwepo kabla ya kutanga ajira hizo mpya.
Naibu
waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI anayeshughulikia Elimu,
Kassim Majaliwa, alisema jana kuwa walimu hao watasambazwa katika shule
za msingi na sekondari nchini.
Alisema
taratibu zote za ajira kwa walimu hao wapya zimekamilika na kwamba mwezi
ujao wote walioajiriwa watakuwa wamepangiwa vituo vyao vya kazi.
Majaliwa
alisema majina ya walimu wote walioajiriwa na vituo vyao vya kazi tayari
kwa kuanza majukumu na serikali itaendelea kuhakikisha uhaba wa walimu
nchini unakuwa historia.
Hata
hivyo alisema kati ya walimu hao wapya 36021 watakuwa chini ya TAMISEMI
na waliobaki watapelekwa kuwa chini ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi.
Aliongeza kuwa kati ya walimu hao wa ngazi ya cheti ni 17,928 stashahada 5416 na wale wa ngazi ya shahada ni 12,677.
Alisema
mgawanyo wa walimu hao uatazingatia na kutoa kipaumbele kwa maeneo na
shule zenye uhaba mkubwa ili kuhakikisha changamoto hiyo inaendelea
kutatuliwa.
"Tumepanga
walimu kulingana na mahitaji ya shule husika ili kuifanya ikama itoshe.
Tumetoa maelekezo kwa maofisa elimu na wakurugenzi nchini kuacha tabia
ya kuwajaza walimu wengi katika kituo kimoja. Tutasimamia kikamilifu
kuwasambaza walimu hao ili kuhakikisha shule zenye uhaba mkubwa zinapewa
kipaumbele," alisema.
Alisema
baada ya kukamika kwa taratibu walimu wapya wanatakiwa kuanza kuripoti
katika vituo vyao vya kazi kuanzia aprili mosi mwaka huu.
Alisema
idadi hiyo inajumuisha walimu wa masomo ya sayansi wa shule za msingi,
sekondari, vyuo vya ualimu na walimu wa elimu maalumu.
Kwa
mujibu wa vyanzo mbalimbali kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
kila mwaka zaidi ya walimu 40,000 huitimu nchini kutoka kwenye vyuo
mbalimbali.
Mwaka
jana serikali ilitoa ajira mpya kwa walimu 26,537 wa shule za msingi,
sekondari na vyuo vya ualimu ambapo mwaka juzi walimu 23,907 waliajiriwa
No comments:
Post a Comment