Sanya Juu ni mji mdogo
ndani ya wilaya Siha Mkoani Kilimanjaro ikiwa ni Km 25 toka Bomang'ombe
na KM 50 toka Moshi Mjini, weekend hii nilifanikiwa kuutembelea Mji wa
Sanya Juu ambapo siku ya Jumamosi mji huu huwa umechangamka kwa
shamrashamra za kibiashara. katika pita pita zangu nilifanikiwa
kulitembelea soko ila nilishangazwa na hali niliyo ikuta ya miundombinu
isiyo kidhi na kulifanya soko kuonekana hatarishi kwawafanya biashara na
wateja wao kiafya.
Huu ni msimu wa mvua kwa
sehemu kubwa ya mkoa wa Kilimanjaro, hatua za haraka zinatakiwa
kuchukuliwa kuimarisha miundombinu ya soko la Sanya Juu kuimarisha afya
za wafanyabiashara na wateja wao.
Na mdau wa matukiodaima.com Bw wito msafiri aliyekuwepo mkoani Kilimanjaro
moshi |
No comments:
Post a Comment