Mkuu wa mkoa wa Iringa, Dr. Christina Ishengoma leo amezungumza na
wafanya biashara wa manispaa ya Iringa katika ukumbi wa community centre
uliopo eneo la Kitanzini katika manispaa ya Iringa, mada kuu ilikuwa
inahusu mgomo wa wafanya biashara kupinga mashine mpya za kutoa risiti
zilizotolewa na TRA ili zitumike katika biashara zao.
baadhi ya wafanya biashara walio hudhuria katika mkutano huo uliofanyika leo.
Mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa Iringa,Bw. Lucas Mwakabunge, akizungumza na wafanya biashara katika mkutano huo.
wafanya biashara hao wakimsikiliza mkuu wa
Mkuu wa
mkoa huyo alisisitiza kuwa elimu inatakiwa kutolewa kwa wafanya biashara
hao kuhusu umuhimu wa mashine hizo kwa kuwa wafanya biashara wengi
wameonesha hali ya kutoridhishwa nazo na hata kufanya maandamano ya nchi
nzima wakipinga matumizi ya mashine hizo na kutaka kendelea kutumia
mfumo wao wa zamani wa kutumia vitabu.
Mkuu wa
mkoa huyo alidai kuwa yeye sio muhusika mkuu wa suala hilo lakini kama
ilivyo, ni wajibu wake kuzungumza na hata kuwasaidia watu wake hivyo
aliwataka wafanya biashara hao fungua maduka kwani kilio chao kimesikika
na serikali inalifanyia kazi suala hilo.
TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI MOTOMOTO(USIPITWEEEE)
TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI MOTOMOTO(USIPITWEEEE)
baadhi ya wafanya biashara waliotoa mawazo yao katika mkutano huo
Wafanya
biashara hao walidai kuwa hawazitaki mashine hizo kwa sasa kwa sababu
haziwapi faida; husan wale wafanya biashara wadogo wadogo ambao kipato
chao ni kidogo kwa kuwa mashine hizo zina gharama kubwa na matengenezo
yake yana gharama kubwa pia hakupewa taarifa za kutosha kuhusu mashine
hizo bali walishtuliwa tu hivyo hawajaridhika na uamuzi huo wa serikali
kupitia TRA.
mwenyekiti
wa TCCIA alipokuwa anafunga mkutano huo na kumshukuru mkuu wa mkoa kwa
uwepo wake katika mkutano huo pia aliwashukuru wafanya biashara hao na
baadhi wananchi kwa kuudhuria kwao mkutanoni hapo.
polisi wa kutuliza ghasia wakiondoka katika eneo hilo la mkutano.
wafanya
biashara hao bado walionekana kutokuwa na furaha baada ya kufungwa kwa
kikao hicho lakini hali ilikuwa kushoto kulia kwani wapo wafanya
biashara walioonekana wakifungua maduka yao wakati maduka mengine
yalikuwa bado hayajafunguliwa.
mwandishi, Riziki Mashaka, Iringa.
Credit Mjengwa.
No comments:
Post a Comment