TIMU
ya Taifa ya Wanawake inaondoka nchini kesho saa mbili asubuhi kwenda
nchini Zambia na ndege ya Kampuni ya Fastjet ikiwa na matumaini ya
kufanya vizuri.
Twiga
stars inakabiliwa na mechi ya kwanza ya mchujo dhidi ya Zambia ya
kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa Wanawake (AWC)
zitakazofanyika baadaye mwaka huu jijini Windhoek, Namibia.
Akizungumza
wakati wa kuwaaga wachezaji wa Twiga, Mgeni rasmi Katibu wa Kamati ya
Olympiki Tanzania, Filbert Bayi alisema kuwa ana imani na timu hiyo
kwani ni ina wachezaji ambao wamekaa pamoja kwa muda mrefu.
“Nakumbuka
2011 timu hii ikiwa na baadhi ya wachezaji ninaowaonana hapa ilishiriki
kwenye mashindano ya Olympiki Afrika hivyo naamini itafanya vizuri”,
alisema Bayi.
Pia Bayi
alisema anampongeza kocha Kaijage kwa kazi yake nzuri ya kufundisha na
kurejesha heshima kwa Twiga kwani wanaonekana nadhifu kama wanawake.
Naye
kocha Kaijage alisema kuwa anashukuru timu yake ipo vizuri kwani
imejiandaa vya kutosha hivyo wana uhakika watakwenda kufanya vizuri.
Naye
nahodha wa timu hiyo, Sophia Mwasikili alisema wanaamini watafanya
vizuri kulingana na mafunddisho waliyoyapata kwa kocha wao ila dua na
sapoti za watanzania zinahitajika ili wafanye vizuri zaidi.
“Sisi
tupo vizuri kuhakikisha tunashinda mchezo huo wa ugenini ili tujiweke
katika nafasi nzuri ya kusonga mbele ila tunawaomba watanzania watupe
sapoti na dua zao”, alisema Sophia
Twiga
Stars inaondoka na kikosi cha wachezaji 19 na benchi la ufundi lenye
watu watano mechi hiyo itakayooanza saa 9 kamili kwa saa za Zambia.
Msafara wa timu hiyo unaongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
No comments:
Post a Comment